HASSAN MWAKINYO APANDA VIWANGO KIMATAIFA, KWA BONGO NI NAMBA MOJA
HASSAN Mwakinyo aliyewahi kuwa namba moja Afrika na wa 14 duniani baada ya kumchapa kwa TKO, Samm Eggington wa Uingereza aliyekuwa bondia namba nane wa dunia kwenye uzani wa Super Welter mwaka 2018, mwanzoni mwa mwaka huu aliporomoka hadi nafasi ya 86 duniani. Amepanda kwa nafasi 14 katika viwango vya ngumi duniani, huku akitajwa kuwa bondia namba moja nchini. Kwa mujibu wa...
YANGA KUINGIA GWAMBINA COMPLEX KWA MTINDO HUU LEO
KOCHA Mkuu wa Yanga, Mrundi Cedric Kaze, amefunguka kuwa licha ya mwenendo usio mzuri walionao wapinzani wao Gwambina FC lakini bado wataingia uwanjani leo Jumanne wakiwa wanawaheshimu. Kaze ameongeza kuwa kinachowafanya waingie wakiwa wanawaheshimu wapinzani wao ni kuwa wapo nyumbani kwao lakini mawazo yake ni kupata pointi tatu mbele yao. Kaze kwa mara nyingine leo Jumanne ataiongoza Yanga kwenye mechi ya Ligi...
SIMBA:TUNAIFUNGA YANGA NOVEMBA 7
BAADA ya kuibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Mwadui, Kocha Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ametamba kuwa kwa namna yoyote lazima wahakikishe wanaibuka na ushindi dhidi ya wapinzani wao Yanga kwenye mchezo wa dabi ya Kariakoo, unaotarajiwa kupigwa Jumamosi hii ya Novemba 7. Mchezo huo awali ulipangwa kupigwa Oktoba 18, mwaka huu kabla ya kusogezwa mbele kutokana na...
KAZE ANA KAZI YA KUPAMBANA NA VIGONGO VITANO VYA MOTO NOVEMBA
KOCHA Mkuu, Cedrick Kaze ana kibarua cha kusaka pointi 15 kwenye mechi zake tano ambazo atakuwa uwanjani na timu yake kwa mwezi Novemba.Uzuri ni kwamba tayari ameshaanza kutengeneza kikosi chake kwanza na leo ana kazi ya kusaka pointi tatu mbele ya Gwambina FC, Mwanza.Kete zake za Oktoba zipo namna hii:-Gwambina v Yanga,Novemba 4.Yanga v Simba, Novemba 7.Yanga v Namungo,...
MARADONA HAYUPO FITI KIAFYA
DIEGO Maradona legendi wa zamani wa timu ya Taifa ya Argentina ameripotiwa kupelekwa hospitali kutokana na kutokuwa fiti kwa afya huku wakigoma kuweka wazi kama anasumbuliwa na Corona.Maradona, mwenye miaka 60, alipelekwa hospitali kufanyiwa vipimo baada ya kujihisi vibaya kutokana na afya yake kutokuwa kwenye ubora.Legendi huyo atakumbukwa kwa uwezo wake ndani ya uwanja pamoja na vituko vyake ambapo...
GWAMBINA FC KUKIWASHA LEO DHIDI YA YANGA
TIMU ya Yanga inashuka uwanjani leo Novemba 3, 2020 kuivaa Gwambina katika mchezo wa kusaka kujiamini zaidi kwa mchezo ujao dhidi ya watani zao, Simba. Usindi wa Yanga leo katika Uwanja wa Gwambia utaifanya timu hiyo kukaa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu kwa raha zaidi licha ya sare pia inaweza kuwapa uongozi hadi matokeo ya Azam FC dhidi ya Dodoma Jiji. Wageni...
KUONA BALAA LA SARPONG NA CHAMA KWA MKAPA BUKU SABA TU
NOVEMBA 7, Uwanja wa Mkapa mchezo wa dabi ya Kariakoo kati ya Yanga na Simba unatarajiwa kupigwa kuanzia saa 11:00 jioni.Viingilio kwenye mchezo huo unaosubiriwa kwa shauku na wadau ili waweze kuona balaa la Michael Sarpong wa Yanga na Clatous Chama wa Simba ni kama ifuatavyo:- mzunguko wa rangi ya kijani ni 7,000( buku saba).Viti vya rangi ya machungwa...
KOCHA YANGA AMFUNGUKIA NYOTA WAKE SARPONG
KOCHA Mkuu wa Yanga, Mrundi, Cedric Kaze, amesema ana imani na mshambuliaji wake, Mghana, Michael Sarpong na hivi karibuni wananchi watamuelewa. Kauli hiyo aliitoa mara baada ya timu hiyo kufanikiwa kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Biashara juzi kwenye Uwanja wa Karume, Musoma. Katika mchezo huo, bao la Yanga lilifungwa na Sarpong dakika ya 68. Akizungumza na Championi Jumatatu, Kaze alisema...
VIWANJA SABA VYAPIGWA PINI NA BODI YA LIGI
BODI ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPLB) leo Novemba 2 imevifungia viwanja viwanja 7 kutotumika kwa ajili ya mechi za mashindano kutokana na kukosa baadhi ya sifa za kikanuni zilizoanishwa zinazozungumzia sheria namba 1 ya mpira.Viwanja hivyo ambavyo vimepigwa pini ili vifanyiwe marekebisho na TPLB itavikagua baada ya marekebisho kukamilika ni pamoja na :-Uwanja wa Majimaji uliopo Songea ambao...
NYOTA KAGERA SUGAR AINGIA ANGA ZA KAGERE
BAADA ya jana, Novemba Mosi kufunga bao lake la nne nyota mzawa, Yusuph Mhilu anaingia anga za Meddie Kagere mshambuliaji namba moja wa Simba.Mhilu alipachika bao hilo dakika ya 69 wakati timu yake ya Kagera Sugar ikisepa na pointi tatu za Mtibwa Sugar Uwanja wa Kaitaba.Bao la kwanza kwa Mtibwa Sugar lilipachikwa na Vitalis Mayanga ingizo jipya ndani ya...