BEKI SIMBA AWEKA REKODI YAKE, MUGALU KAMA KAWAIDA
BEKI wa Simba, Ibrahim Ame ambaye ni ingizo jipya kwa msimu wa 2020/21 akitokea Klabu ya Coastal Union jana Oktoba 17 ameandika rekodi yake kwa kufunga bao lake la kwanza ndani ya kikosi hicho.Licha ya kwamba ni beki, kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa Uwanja wa Azam Complex dhidi ya Mlandege FC ya Zanzibar alipachika bao wakati Simba ikishinda mabao...
TANZANIA KUANDAA MASHINDANO YA AFCON
BARAZA la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa), limeipendekeza Tanzania kuandaa michuano ya kusaka tiketi ya kufuzu kushiriki Mashindano ya Afrika (Afcon) kwa wanawake yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Novemba 22 hadi Desemba 6, mwaka huu jijini Dar. Taarifa hiyo ilitolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Cacafa, Auka Gecheo, Alhamisi, Oktoba 15 wakati wa kikao cha Kamati ya Utendaji ya...
BALE KUKIWASHA LEO SPURS
TOTTENHAM wanatarajiwa kuwa uwanjani leo Oktoba 18 kwa kukipiga dhidi ya West Ham United, ni mchezo wa Premier League na kuna taarifa kuwa Jose Mourinho anaweza kumpa nafasi ya kuanza katika kikosi cha kwanza staa wake, Gareth Bale. Ikiwa Bale atapata nafasi ya kuichezea inamaanisha itakuwa ni mara yake ya kwanza kuanza kukipiga akiwa na jezi ya Tottenham tangu arejee...
MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTI XTRA JUMAPILI
MUONEKANO wa ukurasa wa mbele Gazeti la SPOTI XTRA Jumapili
UKUTA WA MABEKI WA YANGA WAWEKA REKODI NDANI YA LIGI
UKUTA wa Klabu ya Yanga unaoongozwa na nahodha Lamine Moro pamoja na Bakari Mwamnyeto umeweka rekodi Bongo kwa kuwa ni namba moja kwa timu zote 18 zinazoshiriki Ligi Kuu Bara kufungwa mabao machache na kuongoza kwa kufunga mabao mengi.Yanga ikiwa imecheza jumla ya mechi tano ambazo ni sawa na dakika 450 imeruhusu kufungwa bao moja pekee tofauti na ukuta...
POLISI TANZANIA:TUTAFUNGA MABAO MENGI KWA MIPIRA ILIYOKUFA
GEORGE Mketwa, Kocha Msaidizi wa timu ya Polisi Tanzania amesema kuwa mpango mkakati namba moja ndani ya timu hiyo ni kufunga mabao mengi kwa mipira iliyokufa ambayo wamekuwa wakiipata kwenye mechi zao ndani ya ligi.Kwa sasa Polisi Tanzania ipo nafasi ya saba kwenye msimamo ikiwa na pointi 10 baada ya kucheza mechi tano na imefunga mabao sita. Kinara wa...
KIKOSI CHA SIMBA KITAKACHOKIPIGA NA MLANDENGE FC, AJIBU NDANI
KIKOSI cha Simba ambacho kinacheza na Mlandege FC ya Zanzibar mchezo wa kirafiki Uwanja wa Azam Complex, leo Oktoba 17 Ibrahim Ajibu na Bernard Morrison ndani.
EVERTON YAIKOMALIA LIVERPOOL NA KUGAWANA POINTI MOJAMOJA KWENYE DABI
DABI ya leo Oktoba 17 ndani ya Ligi Kuu England ya Merseyside imekamilika kwa Everton kutoshana nguvu ya kufungana mabao 2-2 na kufanya wagawane pointi mojamoja.Liverpool ilikuwa ya kwanza kufunga kupitia kwa Sadio Mane aliyepachika bao dakika ya 3 likasawazishwa na Keane wa Everton dakika ya 19.Mohamed Salah alipachika bao la pili kwa Liverpool dakika ya 72 na kumfanya...
MTAMBO WA MABAO NDANI YA YANGA HUU HAPA
YANGA inayonolewa na Kocha Mkuu, Cedric Kaze baada ya kusaini dili la miaka miwili, jana Oktoba 16 mtambo wa kutengeneza mabao Kwenye kikosi hicho ni Carlos Carinhos raia wa Angola.Kiungo huyo amehusika Kwenye mabao matatu kati ya saba ambayo yamefungwa na Yanga ndani ya Ligi Kuu Bara.Alimpa pasi zote mbili Lamine Moro ilikuwa ni Kwenye mchezo dhidi ya Mbeya...