RATIBA YA LIGI KUU BARA LEO OKTOBA 15
LEO Ligi Kuu Tanzania Bara inaendelea ambapo kutakuwa na michezo miwili kwa timu nne kusaka pointi tatu viwanja viwili tofauti.Ratiba ipo namna hii Oktoba 15:- Gwambina iliyo nafasi ya 14 kwenye msimamo na pointi nne mchezo wake uliopita ilishinda mabao 2-0 dhidi ya Ihefu v Mtibwa Sugar iliyo nafasi ya 12 na pointi tano, mchezo wake uliopita ilifungwa bao 1-0...
KINARA WA PASI ZA MWISHO BONGO LUIS AJIPA KAZI MBILI
KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Luis Miquissone, raia wa Msumbiji amefunguka kwamba ataendelea na kazi ya kutengeneza mabao kwa wenzake ili kuifanya timu hiyo iendelee kupata pointi tatu kwenye mechi zake. Miquissone ameongeza kwamba licha ya kutoa assisti hizo kwa wenzake lakini pia atafunga kwa sababu ni wajibu wake kikosini hapo. Miquissone kwenye Ligi Kuu Bara kwa msimu huu amehusika katika mabao...
KAZE: NAKUJA YANGA KUFANYA KAZI, AFUNGUKA KILICHOMCHELEWESHA
CEDRIC Kaze,amesema kuwa leo anaweza kutua rasmi Bongo kumalizana na Yanga ili aanze kufanya kazi yake mpya kwa kuwa matatizo yake ya kifamilia ameshayaweka sawa.Awali Kaze ilipaswa aje Bongo Agosti 25 kukinoa kikosi cha Yanga akichukua mikoba ya Luc Eymael raia wa Ubelgiji ambaye alifutwa kazi ilishindikana kwa kuwa aliweka bayana kwamba anahitaji muda wa wiki mbili kutatua matatizo...
ISHU YA KUPOTEZA KWA STARS, SAMATTA AKINGIWA KIFUA
BEKI wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ na Klabu ya Mtibwa Sugar, Dickson Job, amesema kuwa nahodha wa Stars, Mbwana Samatta hapaswi kulaumiwa kutokana na matokeo ya kupoteza kwa bao 1-0 kwenye mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Burundi. Stars ilipoteza kwenye mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa uliochezwa Oktoba 11 na Mbwana hakuyeyusha dakika zote 90...
NEYMAR JR AKIKAZA ATAVUNJA REKODI YA PELE
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Brazil, Neymar, amesogea hadi nafasi ya pili ya wafungaji bora wa muda wote kwa kufikisha magoli 64 akiwa nyuma ya mkongwe Pele mwenye magoli 77. Idadi hiyo ameifikisha baada ya kufunga hat trick dhidi Peru ambapo walishinda kwa magoli 2-4 katika kuwania kufuzu Kombe la Dunia nchini Qatar 2022.Nyota huyo wa PSG mwenye miaka 28, amefunga magoli 64...
MASHINE MPYA YA YANGA YAWAPOTEZA NYOTA WOTE SIMBA
SAHAU kuhusu umri wake wa miaka 33, imebainika kwamba thamani ya jembe jipya la Yanga, Saidi Ntibazonkiza raia wa Burundi ni kufuru kwani amewafunika nyota wote wa Bongo wakiwemo viungo wa Simba, Luis Miquissone na Clatous Chama. Kwa mujibu wa mtandao wa Transfer Market, ambao unajihusisha na masuala mbalimbali ya wachezaji ikiwemo thamani zao, Ntibazonkiza ana thamani ya Euro 550,000...
AZAM FC YATUMA UJUMBE HUU KWA MWADUI FC
ABDULKARIM Amin, Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Azam FC amesema kuwa wanahitaji kushinda mechi zao za mbele ikiwa ni pamoja na itakayochezwa kesho dhidi ya Mwadui FC kwa kuweka bayana kwamba wanahitaji pointi tatu kwenye mchezo huo.Tayari Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu, Aristica Cioaba imeshinda mechi tano ndani ya dakika 450 Oktoba 15 itashuka Uwanja wa Azam Complex...
NYOTA SIMBA AWAPA TANO YANGA KUINASA SAINI YA KOCHA MRUNDI
MSHAMBULIAJI wa zamani wa Simba, Mrundi, Laudit Mavugo amefunguka kuwa Yanga ina bahati kubwa ya kuweza kumnasa kocha Cedric Kaze kwa kuwa anaamini sasa wanaweza kucheza soka la pasi katika uwanja wowote wataokwenda kucheza kutokana na kocha huyo kuwa na utalaam huo. Mavugo ametoa kauli hiyo kufuatia uongozi wa Yanga kumalizana na Kaze ambaye anakuja kubeba mikoba ya Mserbia, Zlatko...
KAGERA SUGAR YAZITAKA POINTI TATU ZA NAMUNGO
MECKY Maxime, Kocha Mkuu wa Kagera Sugar amesema kuwa maandalizi ambayo wameyafanya yanawapa uhakika wa kusepa na pointi tatu mbele ya Namungo FC kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara. Leo Oktoba 14, Kagera Sugar inajitupa Uwanja wa Majaliwa kusaka pointi tatu muhimu ikiwa ni mzunguko wa sita baada ya ule wa tano kukamilika.Timu zote zinakutana uwanjani zikiwa na matokeo yanayofanana...
WAHOLANZI WAPEWA JUKUMU LA KUMLETA KOCHA MPYA WA YANGA BONGO
IMEBAINIKA kuwa wakati Mrundi Cedric Kaze, akijiandaa kuja kuchukua mikoba ya kuwa Kocha Mkuu wa Yanga, Waholanzi ndiyo ambao watahusika kumleta kocha huyo hapa nchini. Waholanzi hao kupitia Shirika la Ndege la taifa hilo, KLM Royal Dutch Airlines (KLM), ndiyo watakaombeba Kaze kwa kumtoa Canada alipo kwa sasa na kumshusha katika ardhi ya Tanzania Alhamisi saa 4 usiku, maalum kuanza...