MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI IJUMAA
MUONEKANO wa Ukurasa wa mbele Gazeti la Championi Ijumaa, nafasi ya kushinda ndinga mpya ni yako
BREAKING:CHIRWA AMALIZANA NA AZAM FC, DILI LAKE KUTUA YANGA LABUMA
OBREY Chirwa mshambuliaji wa Azam FC, ameongeza mkataba mpya wa mwaka mmoja kuendelea kusalia ndani ya timu hiyo.Mkataba wa awali wa nyota huyo alioongeza Juni mwaka jana, ulikuwa unamalizika mwishoni mwa msimu huu, hivyo kwa kusaini tena kutamfanya aendelee kusalia hadi mwishoni mwa msimu ujao.Chirwa alikuwa Kwenye hesabu za kurejea Yanga ambayo ilikuwa Klabu yake ya zamani ambayo inaelezwa...
SABABU ILIYOMFANYA CHAMA AKATUA SIMBA HII HAPA
CLATOUS Chama nyota anayekipiga ndani ya Simba amesema kuwa sababu kubwa iliyomfanya akubali kujiunga na klabu hiyo ni malengo ambayo aliyaona kwa mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara.Chama alijiunga na Simba msimu wa 2018/19 akitokea Klabu ya Power Dynamo ya Zambia na msimu wake wa kwanza alitwaa Kombe la Ligi Kuu Bara na kufika hatua ya robo...
SASA YANGA WASHINDWE WENYEWE KWA MTAMBO HUU WA MABAO
SASA Yanga washindwe wenyewe kwa Obrey Chirwa, unaweza kusema kuwa ameshaingiza mguu mmoja! baada ya uongozi wa timu ya soka ya Azam FC, kuanza harakati za kumtafuta mbadala wake.Inaelezwa kuwa Azam wanamtafuta mbadala wake kutokana na mchezaji huyo kudaiwa kuwa katika harakati za kutaka kuondoka klabuni hapo na kurejea Yanga sehemu ambayo alicheza kwa mafanikio makubwa.Mkataba wa Chirwa na...
SAMATTA APATA DILI JINGINE, VILLA WAKISHUKA TU ANAIBUKIA HUKU
BABA mzazi wa mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta, mzee Ally Samatta amefunguka kuwa anaamini mtoto wake ataendelea kucheza Ligi Kuu England hata ikitokea Aston Villa ikishuka daraja kwa kuwa tayari timu ya Everton imejipanga kumchukua.Mshambuliaji huyo amejiunga na Villa kwa mkataba wa miaka minne na nusu katika kipindi cha dirisha dogo akitokea KRC Genk ya nchini Ubelgiji.Mzee...
HIVI NDIVYO KOCHA WA SIMBA ALIVYOUNGANA NA GLOBAL GROUP KUTOA MSAADA
KKOCHA wa zamani wa Simba, Talib Hilal amevutiwa na namna Global Group ambavyo imekuwa ikisaidia jamii na kuamua kushirikiana nayo kufikisha misaada kupitia kampuni hiyo.Kwa sasa Talib ni Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya soka la ufukweni la Oman na safari hii ametoa msaada wa vyakula kama sukari, mchele, tambi na mafuta katika vituo vinne vya watoto yatima...
KWA WALICHOKIFANYA IHEFU WANASTAHILI KUWA DARASA, ILA HILI LA CORONA LISIPUUZWE
KAZI bado ipo palepale kwa kila mmoja kuendelea kujilinda kila siku kila saa kwa kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona.Virusi vya Corona ni janga la dunia nzima kwa sasa hivyo kwa wale ambao bado hawajashtuka ni lazima walitambue hilo kwanza na kuanza kuchukua tahadhari.Tahadhari kwa kila mmoja ni hatua ya kwanza ili kila mmoja aweze kujilinda yeye mwenyewe...
SARRI APEWA ZIGO LA LAWAMA NA KIUNGO HUYU ANAYEKIPIGA BORUSSIA DORTMUND
KIUNGO wa Borussia Dortmund, Emre Can amefunguka kuwa aliyewahi kuwa kocha wake Maurizio Sarri alishindwa kumpa nafasi, lakini kwa kiasi alipata uzoefu.Can amejiunga na Dortmund katika usajili wa dirisha dogo wa Januari akitokea Juventus ambako alikuwa hana nafasi kwenye kikosi cha Sarri.Kiungo huyo kilichomkimbiza zaidi Juventus ni kile kitendo cha kuachwa katika kikosi cha wachezaji ambao walikuwa wanashiriki Ligi...