ZAHERA AMGOMEA KOCHA MPYA YANGA, AANIKA SABABU ZAKE
KOCHA wa Yanga, Mwinyi Zahera amegoma katakata kuchaguliwa kocha msaidizi na viongozi wake huku akiwataka wamuachie hiyo kazi yeye wa kuchagua wa kufanya naye kazi.Zahera ambaye alianza kuinoa Yanga mwishoni mwa msimu wa 2017/18, tangu hapo alikuwa akisaidiwa na Mzania Noel Mwandila ambaye alimkuta kikosini hapo. Yanga hivi karibuni ilihusishwa na mpango wa kuleta kocha msaidizi mpya huku jina...
LISTI KAMILI YA WACHEZAJI 10 WLAIOMWAGA WINO YANGA HII HAPA, SI MCHEZO
LISTI kamili inayotajwa kusajiliwa na Yanga mpaka sasa1. Issa Bigirimana (APR Rwanda)2. Patrick Sibomana- (Mukura Victory Rwanda)3. Mohammed Camara- (Horoya Guinea)4. Mustapha Suleiman- (Aigle Noir AC Haiti)5. Sadney Ukhrob (Namibia)6. Lamine Moro (Ghana)Wachezaji wa ndani1. Ally Mtoni (Lipuli FC)2. Kassim Khamis Abdallah (Kagera Sugar)3. Abdulaziz Makame (Mchezaji Huru)4. Ally Ally (KMC)
HAZARD: NIMEFANYA JAMBO GUMU MAISHANI KUONDOKA CHELSEA
BAADA ya Real Madrid kukamilisha dili la Eden Hazard kutoka Chelsea kwa dau la Euro milioni 150, Hazard amesema amefanya maamuzi magumu kwenye sekta ya michezo.Hazard amekubali kusaini mkataba wa miaka mitano ndani ya Madrid ya Zinedine Zidane na anatarajiwa kufanyiwa vipimo Juni 13.Nyota huyo ametupia jumla ya mabao 110 kwenye michezo 352 baada ya kujiunga na klabu ya Chelsea...
MBIVU NA MBICHI ZA ZITAKAZOSHUKA NA KUPANDA TPL KUJULIKANA LEO
MBIVU na mbichi kwa timu za Ligi Kuu Bara (TPL) Kagera Sugar na Mwadui FC kubaki ama kushuka moja kwa moja itajulikana leo baada ya dakika 90.Kagera Sugar leo itakuwa kibaruani kucheza mchezo wa Playoff na Pamba uwanja wa Kaitaba huku Mwadui FC ikimenyana na Geita FC uwanja wa Mwadui.Timu zote mbili zina kumbukumbu ya kutoka suluhu kwenye michezo...
MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMAMOSI
MUONEKANO wa Ukurasa wa mbele Gazeti la CHAMPIONI Jumamosi
YANGA HAWATAKI UTANI, WANAUTAKA UBINGWA WA LIGI YA MABINGWA AFRIKA
BAADA ya kupata nafasi ya kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Yanga imeweka wazi lengo lao ni kutwaa ubingwa huo msimu ujao.Yanga imepata nafasi ya kushiriki michuano hiyo msimu ujao baada ya kumaliza ligi msimu uliopita ikiwa nafasi ya pili huku Tanzania ikiongezewa nafasi za uwakilishi kutoka nafasi moja hadi mbili.Klabu hiyo imepanga kuitumia hafla ya harambee yake...
SINGIDA UNITED WAJA NA MTINDO MPYA WA USAJILI, WATANGAZA FURSA
UONGOZI wa Singida United umetangaza fursa kwa wachezaji wote ambao wanahitaji kujiunga na kikosi hicho kwa ajili ya msimu mpya wa mwaka 2019/20.Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Singida United, Cales Catemana amesema kuwa lengo la mradi huo ni kutoa fursa kwa wachezaji wote wenye uwezo kuonesha ujuzi wao mbele ya benchi la ufundi."Hii ni fursa maalumu kwa...
KOCHA YANGA AFICHUA SIRI YA MABAO YA KINDOKI
KOCHA wa magolikipa wa kikosi cha Yanga, Juma Pondamali amesema kuwa kikubwa kilichokuwa kinamponza mlinda mlango Klaus Kindoki kushindwa kufanya vizuri ni hofu akiwa langoni.Kindoki ambaye ni chaguo namba moja mbele ya Kocha Mkuu, Mwinyi Zahera msimu wa 2018/19 alikuwa akifanya makosa mengi ya kiufundi hali iliyofanya afungwe mabao kwenye baadhi ya michezo aliyokuwa langoni.Mfano katika michezo ambayo alifungwa...
TAIFA STARS: HAKUNA CHA KUHOFIA TUNAKWENDA KUFANYA MAAJABU
NAHODHA wa timu ya Taifa ya Tanzania, Mbwana Samatta amesema kuwa wanakwenda kufanya maajabu nchini Misri kwa kuwa wanajua wanapeperusha Bendera ya Taifa kwenye michuano ya Afcon nchini Misri.Stars wamekwea pipa leo kuelekea nchini Misri ambapo wanakwenda kuweka kambi kwa ajili ya maandalizi ya michuano hiyo inayotarajiwa kuanza Juni 21.Akizungumza na Saleh Jembe, Samatta amesema kuwa kibarua chao kikubwa...