FT: YANGA SC 3-0 POLISI TZ….MAYELE KAANZA UPYAAAA KUWATETEMESHA…HUYU MZINZE NI WA ULAYA KABISA YANI…
MABINGWA Watetezi Yanga SC wameanza mzunguko wa pili kwa ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Polisi Tanzania mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania bara uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Mabao ya Yanga yamefungwa na Jesus Moloko dakika ya 46,Fiston Mayele dakika ya 77 na Clement Mzinze dakika ya 85. Kwa ushindi huo Yanga wamefikisha Pointi 41...
BAADA YA ISHU YA MPOLE KUISHA…YONDANI NAYE AWANYIMA USINGIZI GEITA GOLD…
Mabosi wa Geita Gold wamekuwa na vikao vya mara kwa mara huku ajenda kubwa ikiwa ni kujadili maboresho ya kikosi chao katika dirisha dogo pamoja na kuanza mikakati ya kuwabakisha wachezaji ambao mikataba yao inaenda ukingoni. Miongoni mwa mastaa ambao mikataba yao inamalizika ni beki mkongwe, Kelvin Yondani ‘Corton Juice’ ambaye taarifa zinadai ameanza mazungumzo mapya licha ya wachezaji wengi...
SIMBA YAJIBU KILIO CHA MASHABIKI….KAZI KUANZA RASMI KESHO…CHAMA MAPEMA TU….
Kikosi cha Simba kinafanya mazoezi jijini Mwanza kujiandaa na mechi tatu mfululizo za Ligi Kuu Bara zitakazopigwa Kanda ya Ziwa, benchi la ufundi na baadhi ya nyota wa timu hiyo wakiwahakikisha mashabiki wanaenda kuvuna pointi tisa za ugenini. Simba itaanza duru la pilikesho Jumapili kwa kuvaana na Geita Gold kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza kabla ya kwenda Mjini...
SIKU CHACHE BAADA YA KUJIUZULU…BARBARA AIBUKA NA HILI JIPYA KUHUSU SIMBA…
Siku chache baada ya kutoa notisi ya kuachia ngazi ndani ya Simba, Ofisa Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo, Barbara Gonzalez ameanza kuwaaga baadhi ya wafanyakazi aliofanya nao kazi klabuni hapo. Barbara ameweka bayana kufikia Januari ataachia ngazi kwenye nafasi hiyo kwa sababu alizozianisha, lakini kabla hajatimiza lengo hilo juzi alifanya hafla fupi na wafanyakazi wote waliokuwa chini yake na kuwaaga...
MWAKINYO: WAZANZIBAR HAWATUTAKI…HUU MUUNGANO UNAUNGANISHA NINI..?
Bondia Hassan Mwakinyo (27) @_hassanmwakinyojr ambaye anajiandaa na pambano lake dhidi ya Bondia Mmarekani Peter Dobson (32) ambalo limepangwa kufanyika Desemba 30, 2022 katika Uwanja wa Mao Tse Tung, Zanzibar, ameelezea masikitiko yake kwa kile alichodai Mabondia wa Zanzibar wameandika barua wakidai hiyo ni fursa ya Wazanzibar na sio ya Watanzania Bara. Pambano hilo la Mwakinyo vs Mmarekani Dobson ni...
KUELEKEA MECHI YA FAINAL KESHO…MBAPPE AOMBA MSAADA WA AFRIKA KUISHINDA ARGENTINA…
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ufaransa Kylian Mbappe amesema kwenye mechi yao ya fainali dhidi ya Argentina anategemea sapoti kubwa kutoka barani Afrika kwa kuwa Wafaransa wengi asili yao ni Afrika. "Nategemea kuona sisi tutakuwa na mashabiki wengi zaidi kutoka barani Africa, tofauti na Argentina ambao wao mashabiki wao ni wale wa Messi,Sisi mashabiki wetu ni watu wote duniani...
YANGA PRINCESS WAMFUTA MAYELE KUWAPA UJANJA WA KUITUNGUA SIMBA QUEENS..
Desemba 22, 2022, mwaka huu ni ‘Derby ya Kariakoo’ kwa upande wa soka la wanawake. Timu ya Yanga Princess itacheza dhidi ya Simba Queens. Yanga Princess wataingia kwenye mchezo huo wa tatu wa Ligi Kuu ya Wanawake msimu huu, wakitoka kuifumua Mkwawa Queens mabao 4-0. Akizungumza, Mratibu wa kikosi hiko, Kibwana Matokeo amesema kikosi hiko kitafanya mazoezi yake mchana leo kwenye...
RASMI….SIMBA WAANIKA ISHU YAO NA BOBOSI ILIVYO….MANZOKI ATAJWA…
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally amefichua ni kweli kuna mipango inafanyika kumhusu Cesar Lobi Manzoki raia wa DR Congo, lakini akaweka wazi kuwa mpaka sasa hakuna lolote kati yao na Bobosi Byaluhanga raia wa Uganda. Manzoki na Bobosi wamekuwa kwenye rada za Simba tangu kipindi cha usajili wa dirisha kubwa ambapo kwa Manzoki, tayari walifikia makubaliano...
NABI: TULIENI…HAO WAARABU TUNAPIGA KAMA KAWA…. WANATOKEA MTAANI KWANGU KABISA…
Kocha Mkuu wa Yanga Mtunisia, Nasreddine Nabi amewaondoa hofu mashabiki wa timu hiyo, kupangwa na US Monastir FC ya nchini Tunisia katika kundi moja hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika. Yanga imepangwa pamoja katika Kundi D, zikiwa na timu za Union Sportive Monastery ya nchini Tunisia, TP Mazembe ya DR Congo na Real Bamako ya huko Mali ambazo...
KISA YANGA….MANULA ‘AWACHANA LIVE’ MASTAA WENZAKE SIMBA…
Kipa namba moja wa Simba, Aishi Manula amesema ili kulirudisha taji la Ligi Kuu msimu huu ni lazima wachezaji wajitoe kwa ajili ya timu. Kipa huyo amesema wachezaji wenzake wa Simba ni lazima wacheze kwa bidii kutokana na ushindani uliopo kutoka Yanga na Azam. Manula amemaliza mzunguko wa kwanza akiongoza kwa kutoruhusu bao mara sita katika michezo 11 aliyodaka kwenye mzunguko...