MCHAWI YANGA HUYU HAWA…STRAIKA SIMBA AICHAMBUA A-Z…NABI NA KAZE MTEGONI…
Pitia ukurasa wa mbele wa Gazeti la MwanaSpoti la leo Jumamosi.
KWA HILI LA MANULA HAPANA AISEE…ISHAKUWA ‘TO MUCH’ SASA…..
Aishi Manula ni kipa mzuri sana. Ana vitu vingi ukilinganisha na makipa wetu wazawa wengine waliopo Ligi Kuu. Kuanzia kwa kina Metacha Mnata, Aboutwalib Msheri, Beno Kakolanya na kadhalika. Kwa muda sasa amekuwa akilinganishwa na kushindanishwa na makipa wazawa na hata wa kigeni, lakini amekuwa kinara na kuwaacha akibaki kuwa namba moja kuanzia Simba hadi timu ya taifa ‘Taifa Stars’. Kulikuwepo...
MWAKALEBELA ‘AMPIGA NA KITU KIZITO’ NABI…”..HATA LIGI TUTATAPOTEZA KWA SIMBA…”
Aliyewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Frederick Mwakalebela, amesema timu hiyo ina kibarua kigumu cha kufuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, lakini amemtaka Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi nguvu na akili nyingine aziongeze katika Ligi Kuu Bara. Kauli hiyo aliitoa kabla ya juzi Jumatano Yanga kucheza mchezo wa kwanza wa Play-Off katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika...
INJINIA HERSI: KUNA WATU WANAIVURUGA YANGA KUPITIA KAULI YA ‘WALA MIHOGO’…
Rais wa Klabu Bingwa Tanzania Bara Young Africans Injinia Hersi Said amekerwa na tabia ya baadhi ya watu wasiotakia mema klabu hiyo, kwa kutumia kauli yake aliyoitoa jijini Mwanza mwishoni mwa juma lililopita alipozungumza na Wanachama. Hersi Said ameonyesha kukerwa na hilo, alipozungumza na Wanachama na Mashabiki wa Young Africans kupitia Yanga TV jana Alhamis (Novemba 03), kuhusu mambo mbalimbali...
OKWA: TOKA NIMEJIUNGA NA SIMBA NAKUMBANA NA MAJERAHA SANA…NASIKIA MENGI TU….
Simba ipo kambini ikiendelea kujifua kwa ajili ya mechi yao ijayo dhidi ya Singida Big Stars, huku mshambuliaji wa timu hiyo, Mnigeria Nelson Okwa akifunguka juu ya kutoonekana uwanjani na kushindwa kufanya mambo tangu atue klabu hapo. Okwa aliyesajiliwa na Simba msimu huu akitokea Rivers United ya Nigeria, hajaonekana uwanjani kwa muda mrefu na kuzua hofu kwa mashabiki Lakini, nyota huyo...
MAYELE KUIPA YANGA ZAIDI YA MIL 600 …JAMBO LITIKI TU BASII…ISHU NZIMA IKO HIVI…
Yanga juzi ilibanwa na Club Africain na kutoka suluhu katika mchezo wa kwanza wa play-off ya Kombe la Shirikisho Afrika, uliopigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, lakini mastaa wa timu hiyo wamebakiwa na dakika 90 za ugenini ili kujihakikisha zaidi ya Sh 600 milioni. Fedha hizo ni kwa timu itakayoingia makundi ya michuano hiyo, ingawa Yanga italazimika kupambana kiume na...
AKAMINKO APELEKWA SIMBA NA YANGA…APEWA NAMBA KIKOSI CHA KWANZA
Kiungo James Akaminko ni kama anazigonganisha Simba na Yanga baada ya mastaa wa zamani wa timu hizo kuonyesha wazi wanatamani akacheze katika klabu zao. Akaminko, raia wa Ghana mwenye umri wa miaka 26 alijiunga na Azam msimu huu kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Great Olympic ya Ghana. Starika wa zamani wa Yanga, Moro United na Prisons, Hery Morris alisema Akaminko...
KISA UZITO WA SHABANI DJUMA…KOCHA YANGA AMUUMBUA ZAHERA…AFUNGUKA A-Z UKWELI WA JAMBO…
Beki wa kulia wa Yanga, Shaban Djuma yuko kwenye wakati mgumu akionekana kama kwa sasa amekuwa ‘njia’ ya mashambulizi kupitia kwake kutokana na kinachodaiwa kuongezeka uzito, lakini kocha ameibuka na kumtetea huku akifafanua kitaalamu. Kocha wa mazoezi ya viungo wa Yanga, Helmy Gueldich amesema kuwa kwa mujibu wa vipimo vya uzito wanavyofanya mara kwa mara Djuma yuko katika uzito wake...
KISA KIPIGO CHA GOLI 5 BILA KUTOKA SIMBA….KOTEI AIBUKA NA HAYA MAPYA MTIBWA SUGAR…
Licha ya kupokea kichapo cha mabao 5-0 kutoka kwa Simba, kiungo James Kotei amesema Mtibwa Sugar inaonyesha mwanga wa kufanya vizuri msimu huu kulinganisha na ule uliopita walioponea chupuchupu kushuka daraja. Kotei anayecheza kwa mkopo Mtibwa Sugar akitokea Singida Big Stars, alisema uwepo wa nyota wenye kiwango bora katika kikosi cha timu hiyo umeifanya iwe na uhakika wa kupata matokeo...
INJINIA HERSI: MASHABIKI YANGA WANATUKOSEA SANA…WANATUVUNJA MOYO…
Rais wa Klabu ya Yanga, Injinia Hersi Saidi amesema pamoja na timu kukosa ushindi dhidi ya Club African katika mchezo wa kwanza kufuzu hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika lakini bado haijakata tamaa. Hersi amesema wachezaji pamoja na benchi la ufundi walitumia kila mbinu ndani ya uwanja lakini ilishindikana na kwamba bado wana matumaini ya kufanya vizuri katika mechi...