KISA YANGA KUPATA SARE JANA…NABI ‘ANG’ATWA SIKIO’…MGUNDA YEYE NA REKODI TU…
Pitia ukurasa wa mbele wa gazeti la SpotiXtra la leo Alhamisi.
KANOUTE NA JAMBO LAKE KWA MGUNDA…STRAIKA AFICHUA SIRI KATI YAO…YANGA WAPEWA ‘NDIMU’ MARUDIANO…
Pitia ukurasa wa mbele wa gazeti la MwanaSpoti la leo Alhamisi.
SIMBA YAANZA KUZITAFUTA 5-0 ZINGINE KWA AJILI YA SINGIDA BIG STARS…
Baada ya kushinda mabao 5-0 dhidi ya Mtibwa Sugar, kikosi cha Simba kimeingia kambini leo mchana jumatano kujiandaa na mchezo mwingine wa ligi. Kikosi cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Juma Mgunda kiliichapa Mtibwa Sugar Oktoba 30, mwaka huu kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar. Simba inatarajia kucheza mchezo ujao wa ligi kuu Novemba 9 mwaka huu dhidi ya Singida Big Stars...
BECKHAM NA INTER YAKE WAMKOMALIA MESSI…WATAKA JAMBO LIWE HARAKA…
Inter Miami imeongeza nguvu ya kutaka kumsajili Lionel Messi baada ya kumalizika kwa Kombe la Dunia. Nyota huyo wa kimataifa wa Argentine mwenye miaka 35, anaingia katika mwaka wa mwisho wa mkataba wake ndani ya Paris Saint-Germain. Wakati miamba hiyo ya Ligue 1 ikitaka kumbakiza, gazeti la The Athletic kwa mshangao liliandika jana kuwa klabu inayomilikiwa na David Beckham ya Ligi...
KARIA : MTANIKUMBUKA…SITAKUFA NITABAKI NIKIWATAZAMA…
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania ‘TFF’ Wallace Karia amesema anakubali na kupokea lawama zote zinazoelekezwa kwake kuhusu mwenendo mzuri na mbaya wa Soka. Rais Karia ametoa kauli hiyo leo Jumatano (Novemba 02), alipozungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es salaam, wakati wa hafla ya kusaini mkataba ba Kampuni ya Ndege ya Precision Air. Kiongozi huyo amesema kwa muda alioongoza...
FT: YANGA 0-0 CLUB AFRICAIN ….HAKUNA CHA TUISILA WALA AZIZI KI….NABI PRESHA INAPANDA….
DAKIKA 90 za mchezo wa kwanza wa mchujo kuwania nafasi ya kutinga hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika kati ya Yanga dhidi ya Club Africain zimemalizika kwa suluhu (0-0) kwenye uwanja wa Mkapa na hizi ni dondoo zake. Mwamuzi Celso Armindo Alvacao raia wa Msumbiji hii ilikuwa mara yake ya pili kuchezesha mchezo wa Kimataifa kwenye uwanja wa...
KARIA : AZAM TV SIO WADHAMINI WETU….
Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Walace Karia amesema wapo kwenye mazungumzo na kampuni mbalimbali kwa ajili ya udhamini wa Kombe la TFF. Akizungumza na Waandishi wa Habari, Karia amesema kombe hilo halina mdhamini mkuu na hata kuitwa kombe la Shirikisho Azam ni kutokana na kutokuwa na mdhamini mwingine. “Kombe linaitwa Azam kwa sababu tulisaini nao mkataba wa kuonyesha matangazo...
BAADA YA YANGA KUSHINDWA KULIFURAHISHA TAIFA LEO…KAZI YATUA KWA SIMBA QUEENS…
Mechi ya kwanza ilikuwa ni ya kusoma mashindano lakini Simba Queens wametamba kwamba leo ndio wanaanza mashindano. Juzi walifungwa bao 1-0 na FAR Rabat ya Morocco huku wakikiwasha na Determine Girls ya Liberia. Huo ni mchezo wa pili Kundi A kwenye michuano hiyo ya Ligi ya Mabingwa Afrika iliyojizolea umaarufu mkubwa kwenye wiki za hivi karibuni kutokana na mashabiki kuvutiwa...
YANGA vs CLUB AFRICAIN:…FANYEENI YOOTEE LAKINI HILI LA MWAMUZI MKILISAHAU IMEKULA KWENU….
Hakuna lugha yoyote ambayo mashabiki, wanachama wa Yanga na Watanzania wanataka kusikia leo saa 10 jioni kwenye mechi dhidi ya Club Africain zaidi ya ushindi mnono ndani ya Uwanja wa Mkapa. Hilo ndiyo pekee linaloweza kuiweka Yanga kwenye nafasi nzuri ya kufuzu makundi ya Kombe la Shirikisho na kupooza machungu ya kutolewa katika Ligi ya Mabingwa Afrika wiki chache zilizopita. Wachezaji...
ALLY KAMWE: HATUNA MAHUSIANO NA SIMBA…HATUNA MPANGO NAO HATA…
Afisa Habari wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans Ally Kamwe amesema kamwe klabu yao haitathubuti kuomba ushauri kwa watani zao Simba SC, ili ifanikiwe Kimataifa. Wadau wengi wa Soka nchini Tanzania wamekua wakiushauri Uongozi wa Young Africans kuomba ushauri kwa wenzao wa Simba SC ili wafanikiwe Kimataifa, kutokana na klabu hiyo ya Msimbazi kuwa na mafanikio ya kufika...