TANZANIA U-20 WAANZA SAFARI YA MATUMAINI KUFUZU AFCON….
Kikosi cha Timu ya Taifa ya Wanaume chini ya miaka 20 ‘Ngorongoro Heroes’ kimeondoka leo Alhamis (Oktoba 27) kuelekea Sudan, kwenye michuano ya kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika (U-20 AFCON), kupitia Kanda ya Afrika Mashariki na Kati ‘CECAFA’. Shirikisho la Soka nchini Tanzania ‘TFF’ imethibitisha kuondoka kwa kikosi cha ‘Ngorongoro Heroes’ kupitia kurasa zake za Mitandao ya kijamii. Taarifa iliyochapishwa...
A-Z JINSI YANGA WALIVYOIFANYIA ‘UNDAVA’ KMC JANA….MAMBO HAYAKUWA MARAHISI HIVYO…
BAO pekee la kiungo Feisal Salum alilofunga dakika ya 80 limetosha kuipa pointi tatu katika mchezo wao dhidi ya KMC. Mchezo huo KMC ilitawala dakika 45 za kipindi cha kwanza na kufanya mashambulizi mengi langoni kwa Yanga licha ya kutoweka moira wavuni. Kipindi cha pili Yanga ilifanya mabadiliko ya kuwatoa Bakari Mwamnyeto, Tuisila Kisinda na Dickson Ambundo huku wakiingia Feisal Salum,...
AHMED ALLY: HATUKUPATA TULICHOTAKA KWA YANGA…TUNAHASIRA NA SARE…
KLABU ya Simba imesema haikupata ilichostahili kwenye mechi dhidi ya Yanga, hivyo sasa hasira zao wanazihamishia kwenye mechi dhidi ya Azam FC keshokutwa, Alhamisi katika Uwanja wa Benjamin Mkapa. Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally, amesema mioyo ya wanachama na mashabiki wa timu hiyo imekunjamana na hawana furaha hata kidogo kutokana na kutoka sare ya bao...
BOSI WA SOKA UGANDA ATIA NGUMU MICHO KUTUA JANGWANI…MWENYEWE ADAI YANGA NI FAMILIA YAKE..
WAKATI Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Uganda, Milutin Sredojevic 'Micho', akihusishwa na kuja kurithi mikoba ya Mtunisia Nasreddine Nabi katika kikosi cha Yanga, Mserbia huyo ameanika kila kitu kuhusu tetesi hizo zilizosambaa kwa kasi baada ya kuonekana Uwanja wa Benjamin Mkapa juzi akiwa viongozi wa klabu hiyo juzi. Micho alikuwa miongoni mwa wageni kutoka nje waliohudhuria 'Dabi' ya...
PAMOJA NA KUWA BOSI WA MICHEZO NCHINI…ALLY MAYAI AMPA UFALME MOSES PHIRI…
ALIYEKUWA nahodha wa Klabu ya Yanga na Timu Taifa (Taifa Stars), ambaye kwa sasa ni Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo nchini, Ally Mayayi Tembele, amempa alama zote mshambuliaji wa Simba, Moses Phiri kuwa ndiye nyota wa mchezo wa watani wa jadi Simba na Yanga juzi zilitoka sare ya bao 1-1 katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa kwenye Uwanja...
SADIO MANE ALIVYO’IZIKA’ BARCELONA JANA…ATUNGUA GOLI LA MAPEMA ZAIDI…
HALI ilikuwa mbaya kwa Barcelona kwenye mchezo wa UEFA Champions League ndani ya dakika 90 kwa kuwa hakuna shuti hata moja walilopiga likalenga lango. Katika mashuti 9 waliyopiga ilikuwa ngumu kupenya kwenye ngome ya Bayer ya Msenegal Sadio Mane ambaye alianza kuwatungua dakika ya 10 kwenye mchezo huo. Licha ya kuwa walikuwa Uwanja wa Camp Nou walishuhudia wakichapwa mabao 3-0 na...
RASMI…OUATTARA AJITOA SIMBA….MGUNDA AMPOTEZEA…KASEJA AFANYA UAMUZI MGUMU…
Pitia ukurasa wa mbele wa gazeti la MwanaSpoti la leo Alhamis.
SIMBA WANA JAMBO LA SIRI NA NABI…MWENYEWE AWAPA MASHARTI YANGA….
Pitia ukurasa wa mbele wa gazeti la SpotiXtra la leo Alhamis.
WAKATI AKIZINGUA MAN UTD….RONALDO AKAMILISHA UJENZI WA HOTEL LA KIFARAHI MOROCCO…
Hoteli ya kifahari ya mwanasoka Mreno Cristiano Ronaldo iliyoko Marrakech, Morocco, imeanza kuwakaribisha wageni, kwa mujibu wa chombo cha habari cha Uhispania Europa Press. Hoteli ya kifahari ina vyumba 174 vyenye ukubwa 42 m² nafasi ya biashara, kituo cha biashara chenye 4,500 m2, na kliniki ya kifahari. Hoteli ya Pestana CR7 imejengwa katikati mwa Bustani ya Hay Menara kwa gharama...
FT: YANGA 1-0 KMC FC ….FEI TOTO AMUOKOA NABI DK ZA MCHANA…MAYELE AKOSA REKODI MPYA…
KLABU ya Yanga imeendeleza na rekodi yake ya kutokufungwa katika mechi ya 44 mara baada ya leo kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya KMC Fc. Yanga Sc imeingia uwanjani huku ikiwapumzisha wachezaji wake kadhaa akiwemo Mayele ambaye hakuwepo hata benchi, Feisal Salum ambaye aliingia na kufunga bao dakika ya 80 na kuisaidia timu yake kuondoka na ushindi, Moloko ambaye...