KISA YANGA…MO DEWJI AMTANGAZIA MINOTI MGUNDA…WADAI WAMECHOKA KUFUNGWA…
Pitia ukurasa wa mbele wa gazeti la Championi la leo Ijumaa.
KUELEKEA KARIAKOO DABI….MO DEWJI AMFUNIKA VIBAYA MNOO GSM…AWEKA MEZANI MIL 500 CASH…
Kuelekea kwenye mchezo wa Kariakoo Dabi, Rais wa Heshima wa Simba, Mohammed Dewji ‘Mo’, ameahidi zaidi ya Sh 500Mil kwa wachezaji na benchi la ufundi kuhakikisha wanashinda pambano hilo ili wasivuruge furaha ya kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Jumapili hii, Yanga atakuwa mwenyeji katika mchezo wa Ligi Kuu Bara, ambapo atawakaribisha watani wake Simba, baada ya...
WATZ WALIOTIKISA ‘GOT TALENT’ WAFUNGUKA WALIPOANZIA…WADAI HAIKUWA RAHISI..
Watanzania Ibrahim Ramadhan na Fadi Ramadhan almaarufu Ramadhan Brothers, waliong'ara katika mashindano ya Australia’s Got Talent yaliyofanyika usiku wa Jumapili, Oktoba 16, 2022, wamefunguka mambo mengi kuhusu maisha yao ikiwemo jinsi walivyoanza sarakasi. Ramadhan Brothers wamesema walianza sarakasi tangu wakiwa watoto wadogo lakini walikuwa wakicheza mitaani mpaka walipokuja kugunduliwa vipaji vyao na kocha wao ambaye ndiye aliyewaunganisha kimataifa. Ramadhan Brothers wamepita...
KUELEKEA MECHI YA KARIAKOO DABI…OKRAH NA PHIRI WAAPA ‘KUIHEMEA’ YANGA…
Achana na ushindi walioupata Simba dhidi ya Primeiro de Agosto na kuwavusha hatua ya makundi, unaambiwa kikosi hicho kwa sasa akili zao wamezielekeza mechi dhidi ya Yanga itakayopigwa Jumapili hii katika Uwanja wa Mkapa. Mchezo huo unasubiriwa kwa hamu kutokana na upinzani ulipo baina ya miamba hii kwa sababu ya historia zao, huku kila mmoja akitaka kushinda ili kuwafurahisha mashabiki...
KISA KUPIGWA KIZEMBE NA WASUDAN…SALEH JEMBE NAYE AWAPA ZA USO YANGA SC….
Mchambuzi wa soka nchini, Saleh Ally 'Jembe' amesema ni wakati sasa kwa Timu ya Yanga kufanyia kazi nafasi wanazotengeneza hasa katika mashindano ya kimataifa kwa sababu nafasi za kufunga huwa zinakuwa chache. Baada ya kutolewa na Al Hilal ya Sudan kwenye ligi ya Mabingwa Afrika nakuangukia kwenye Kombe la Shirikisho na wamepangwa kucheza na Club Africain ya Tunisia Novemba 2,...
WALIOPIGWA GOLI 7-0 NA WATUNISIA..WAIPA UJUMBE HUU YANGA…INJINIA HERSI ABAKI ‘AKIKODOA MACHO’…
Ratiba ya Kombe la Shirikisho Afrika imetoka juzi mchana na Yanga imepangwa kuanza na Club Africain ya Tunisia, lakini Kocha wa Kipanga FC ya Zanzibar, Hassan Abdulrahman amewapa faili zima ili watinge makundi. Kipanga ilikutana na Club Africain katika mechi mbili za hatua ya mtoano kabla ya kukutana na nyumbani walilazimishwa suluhu kabla ya kupoteza vibaya kwa mabao 7-0 ugenini...
KISA CAF….MAYELE AWA HABARI YA MJINI TUNISIA…MASHABIKI TUMBO JOTO…
Baada ya Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’ kupanga Droo ya Michezo ya Mtoano ya Kombe la Shirkisho juzi Jumanne (Oktoba 18), baadhi ya mashabiki wa Club Africain ya Tunisia wameonesha hofa yao kwa Mshambuliaji wa Young Africans Fiston Kalala Mayele. Kupitia maoni (comment) katika ukurasa wa timu hiyo baadhi ya mashabiki wameonesha hofu yao kwa Mshambuliaji huyo kwa kuandika...
KISA SIMBA….KOCHA YANGA AKATAA KWENDA UWANJANI KUTAZAMA DABI YA KESHO KUTWA…
Aliyewahi Kuwa Kocha Mkuu wa Young Africans kati ya Mwaka 2009-2011 Kosatdin Papic amesema anatarajia kuona soka safi Jumapili (Oktoba 23), pale Manguli wa Soka la Bongo watakapocheza Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam. Young Africans inatarajia kuwa mwenyeji wa Simba SC katika mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, huku ikijidai Rekodi ya kutopoteza mchezo wowote wa...
BAADA YA YANGA KUTOLEWA LIGI YA MABIGWA…SHAFFIH DAUDA KAIBUKA NA HILI JIPYA …
Mchambuzi wa masuala ya soka nchini, Shaffih Dauda amewapongeza Klabu ya Yanga kwa hatua waliopiga katika michuano ya Kimataifa huku akisema kuwa ni hatua nzuri kwani mafanikio hayaji siku moja. “Naona Yanga wanakwenda vizuri, wana utulivu, wana timu nzuri, suala la matokeo ni jambo la mchakato sio jambo la kulala na kuamka hususan huku kwenye mashindano ya CAF. “Wametolewa na Al...
MO DEWJI AAMUA KUIKOMESHA YANGA…MASTAA SIMBA WAOGA NOTI…ATAKA KIKAO CHA HARAKA NA MGUNDA…
Baada ya kuwaondoa Primiero de Agosto kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika wachezaji wa Simba wameanza mazoezi kujiandaa na mechi ya Yanga Jumapili. Lakini kabla hawajatia mguu uwanjani akaunti zao zitakuwa zimetuna. Bilionea, Mohammed Dewji ‘Mo’ ameamua kukomesha baada ya kuhakikisha akaunti wachezaji zinanona kabla ya kufikia jioni ya leo, kutokana na ushindi bao 1-0 dhidi ya Agosto uliowapeleka kwa kishindo...