Habari mwanamichezo mwenzangu kutoka Dar es salaam leo ni asubuhi nyingine nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika magazeti ya michezo
Habari mwanamichezo mwenzangu kutoka Dar es salaam leo ni asubuhi nyingine nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika magazeti ya michezo
BENCHI la Ufundi la Simba chini ya Kocha Mkuu, Mbrazili, Roberto Oliveira ‘Robertinho’ linafikiria kumuondoa kikosi cha kwanza kiungo mkabaji Sadio Kanoute, ili nafasi yake ichukuliwe na Fabrice Ngoma.
Ngoma raia wa DR Congo, ni kati ya wachezaji wapya waliosajiliwa...
SIMBA bado iko sokoni na sasa imepanga kumshusha kiungo mkabaji, Efoe Novon raia wa Togo huku wakipanga kumtoa kwa mkopo straika wao raia wa Zambia, Moses Phiri.
Novon kwa sasa anaitumikia Klabu ya ASKO Kara ya kwao Togo, ambayo alijiungana...
MSHAMBULIAJI wa zamani wa Yanga, Fiston Kalala Mayele amesema kuwa licha ya Yanga kupoteza kwa kushindwa kubeba Ngao ya Jamii mbele ya Simba anaamini bado timu hiyo ina uwezo mkubwa wa kutwaa ubingwa wa ligi kuu kutokana na ubora...
MABOSI wa Yanga, wameiangalia safu yao ya ushambuliaji katika michezo ya Ngao ya Jamii, fasta wakachukua uamuzi wa kumrudia mshambuliaji wa Al Hilal ya Sudan, Mkongomani, Makabi Lilepo.
Awali Yanga ilifanya mazungumzo na mshambuliaji huyo, ambaye walitaka kumsajili katika usajili...
Michuano ya Magembe Cup inayoendelea mkoani Tabora Kaliua imepata neema kutoka kampuni bingwa ya michezo ya kubashiri ya Meridianbet ambayo imegawa vifaa vya michezo ambavyo ni mipira pamoja na jezi.
Kupitia michuano hiyo inayofanyika wilaya ya Kaliua mkoani Tabora imeendelea...
Beki wa Richardsbay FC, inayoshiriki Ligi Kuu ya Afrika Kusini, Mtanzania Abdi Banda amesema haoni ubaya kusajiliwa wachezaji wengi wa kigeni, ila anaona itofautishe na mipango ya timu ya taifa.
"Wachezaji wa kigeni wanakuja kutupa changamoto wazawa, lakini idadi ya...
Wakati Simba ikitoka na ushindi wa mabao 4-2 mbele ya Mtibwa Sugar katika Uwanja wa Manungu Mkoani Morogoro.
Wachambuzi wengi wa michezo wamezungumzia kiwango cha beki wa kati wa Simba Che Fondoh Malone ambae jana alionekana kufanya makosa mengi yaliyoigharinu...
Ofisa Habari wa Klabu ya Young Africans Sports, Alikamwe amesema kuwa watakachokwenda kukifanya dhidi ya wapinzani wao ASAS FC siku ya Jumapili zitakuwa ni salamu tosha kwa Afrika na kuitambua timu hiyo.
“Tunachokwenda kukifanya Jumapili dhidi ya ASAS FC inatakiwa...