Juzi Emmanuel Okwi aliandika katika mtandao wake wa Instagram kuwa neno kwa heri ni neno chungu sana.
Maneno ambayo yaliweka mjadala kuhusiana na Emmanuel Okwi kuendelea kuwepo Simba. Leo hii Simba imedhibitisha kuwa Emmanuel Okwi siyo mchezaji wao.
Akizungumza na mtandao huu , mkuregenzi mtendaji wa Simba, bwana Magori amedai kuwa Emmanuel Okwi ameshamaliza mkataba na Simba.
Alipoulizwa kuhusu tetesi za Emmanuel Okwi kutakiwa na Kaizer Chiefs ya Afrika kusini amedai kuwa hana hizo taarifa hizo.
“Hizo habari hata Mimi sizijui kama wewe, labda uzungumze na mchezaji mwenyewe ambaye kashamaliza mkataba na Simba”.
” Sijapata hiyo barua, ninachojua Emmanuel Okwi alimaliza mkataba, tukakaa naye akaomba aende kwanza Afcon na akitoka tuendelee na mazungumzo naye”.
“Na mpaka sasa hivi kwenye mikono yake amedai kuwa ana ofa tatu mpaka sasa hivi, hivo tumemwacha aende Afcon, akirudi tutazungumza naye”.Alimaliza kuongea mkurugenzi huyo mtendaji wa Simba
The post Okwi sio mchezaji wa Simba! Kaizer Chiefs yahusika appeared first on Kandanda.