Home Uncategorized Mechi yetu na Azam FC ilikuwa ya kirafiki- Zahera

Mechi yetu na Azam FC ilikuwa ya kirafiki- Zahera

 

Jana katika uwanja wa Taifa kulikuwa na mechi kati ya Yanga na Azam FC, mechi iliyomalizika kwa Azam FC kushinda goli 2-0.

Baada ya mchezo huo kocha mkuu wa Yanga amedai kuwa mechi hiyo ilikuwa ni kama ya kirafiki kwa sababu wachezaji walikuwa wanacheza wanavyojisikia.

” Mechi haikuwa na ushindani, wachezaji walikuwa wanacheza bila maelekezo. Unaona Makambo anabaki na kipa lakini hakuna anachokifanya”.

Alisema kocha huyo ambaye amewezesha timu hii kushika nafasi ya pili licha ya matatizo mengi ya timu yake ya Yanga.

The post Mechi yetu na Azam FC ilikuwa ya kirafiki- Zahera appeared first on Kandanda.

SOMA NA HII  RUVU YAKOMAA KUBAKI TP, MATOKEO NA TIMU ZILIZOSHUKA DARAJA HAYA HAPA