Home Uncategorized YANGA WAPEWA BURE MBADALA WA MAKAMBO

YANGA WAPEWA BURE MBADALA WA MAKAMBO


UONGOZI wa Mwadui FC umesema kuwa upo tayari kuwapa nyota wao Salum Aiyee hata bure endapo watakuwa wanahitaji saini yake msimu ujao.

Yanga kwa sasa inatafuta mbadala wa Heritier Makambo ambaye amesepa Yanga akiwa amefunga jumla ya mabao 17 msimu huu na kujiunga na kikosi cha Horoya ya Guinea huku Aiyee akiwa na mabao 18.

Katibu wa Mwadui FC, Ramadhan Kilao amesema kuwa kwa sasa ahawajona dalili za Yanga kumfuata nyota huyo kama ikitokea wataketi kuzungumza juu ya mkataba wake.

“Unajua maisha ya mchezaji ni mpira sasa kama Yanga watakuwa siriazi kuipata saini ya Aiyee tupo tayari kuwapa bure ila wawe na masalahi bora kwa mchezaji.

“Kwa sasa tunaendeea kupambana ambapo tunakwenda kumenayan a Geita mchezo wetu wa play off tutapambana kupata matokeo na kubaki kwenye ligi msimu ujao,” amesema.

SOMA NA HII  SIMBA YATOA TAMKO LA KIBABE KUHUSU YANGA