Home Uncategorized SIMBA: HAIKUWA RAHISI KUFIKA HAPA

SIMBA: HAIKUWA RAHISI KUFIKA HAPA


KOCHA Mkuu wa Simba, Patrick Aussems amesema kuwa haikuwa kazi rahisi kwao kutwaa ubingwa kwani walicheza mfululizo hasa kipindi cha mwisho ila juhud zimewapa walichokuwa wanastahili.

Aussems amesema kuwa wachezaji wake walikuwa wamechoka kutokana na kucheza michezo 15 ndani ya siku 30 ila hawakuwa na jinsi zaidi ya kutafuta matokeo.

“Haikuwa safari nyepesi kufika hapa, tumecheza michezo mingi ile ya karibu ikiwa ni 15 ndani ya siku 30 ni ngumu sana kupata matokeo chanya muda wote.

“Kwa upande wa waamuzi muda wote nimekuwa nikiona wakifanya majukumu yao ila sikupaswa kujali kwa kuwa wanatimiza majukumu yao ingawa kuna wakati walikuwa wanafanya maamuzi ambayo yanatuumiza sisi pamoja na wapinzani wetu,” amesema.

SOMA NA HII  UONGOZI SIMBA WAWEKA SAWA SUALA LA MGAO WA MAMILIONI YA SAMATA ASTON VILLA