Uncategorized

YANGA YATAJA KILICHOIPONZA KUKOSA UBINGWA MSIMU HUU

admin May 28, 2019 11:09 pm


KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kuwa T-Shirti lake alilokuwa analipenda kuvaa msimu huu halina bahati ya kubeba ubingwa hivyo msimu ujao atabadilisha ili abebe ubingwa.

Yanga jana wamepoteza mchezo wao wa mwisho mbele ya Azam FC kwa kufungwa mabao 2-0 mchezo uliochezwa uwanja wa Taifa.

Zahera amesema kuwa sababu kubwa ya kuvaa T.Shirt hiyo ni nembo yake ambayo ameiteua msimu huu.

“Kila mmoja ana mtindo wake unaomtambulisha hivyo kwangu mimi T.shirt yangu ni utambulisho wangu pamoja na hii kofia, ila sasa nimeona haikuwa na bahati msimu ujao nitaboresha zaidi.

“Tumefungwa kwa kuwa wachezaji hawakuwa na morali kubwa ila hakukuwa na chochote cha kupoteza ila ni matokeo tu yametokea tumepoteza,” amesema Zahera.

SIMBA: HAIKUWA RAHISI KUFIKA HAPA MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMATANO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6131

Leave a Reply