Home Uncategorized STARS KUMENOGA, DOZI MARA MBILI KWA SIKU

STARS KUMENOGA, DOZI MARA MBILI KWA SIKU

KIKOSI cha timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kimeanza mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya Afcon itakayofanyika nchini Misri mwezi Juni.

Stars kwa sasa imeweka kambi ya ndani kwa muda wa wiki moja ambapo baada ya kumaliza program ya mwalimu watakwea pipa kuelekea nchini Misri kuweka kambi mpaka siku ya mashindano.

Kwa sasa Stars wanafanya mazoezi uwanja wa Taifa asubuhi na jioni chini ya kocha mkuu, Emanuel Ammunike.

SOMA NA HII  YANGA WATIBUA MBINU ZA TOWNSHIP ROLLERS NAMNA HII