MEI 28 Ligi Kuu Bara ilifika tamati ambapo bingwa wa ligi msimu wa 2018/19 ni Simba baada ya kumaliza ligi akiwa na pointi 93.
Timu mbili ambazo zimeshuka ni pamoja na Stand Unite na African Lyon huku mbili zitacheza playoff ambazo ni Mwadui FC itamenyana na Geita FC huku Kagera Sugar wakali wa takwimu watamenyana na Pamba ili kumpata mshindi baada ya mchezo wa kwanza wote kutoshana nguvu.
Hzi hapa ni namba ambazo zilibamba ndani ya ligi kuu kama ifuatavyo:-
11
Idadi ya kinara wa mabao ndani ya kikosi cha matajiri wa Dar es Salaam Azam FC yaliyofungwa na Donald Ngoma, huku Obrey Chirwa akifunga jumla ya mabao 3 sawa na nafasi ya kikosi hicho iliyomaliza msimu huu ikiwa na pointi 75.
23
Idadi ya mabao ya mfungaji bora ndani ya Ligi Kuu Bara, Meddie Kagere wa Simba akiifunika ile ya msimu wa mwaka 2017/18 ya Emmanuel Okwi aliyemaliza akiwa na mabao 20.
96:27
Bao la usiku msimu uliopita lilifungwa na Hassan Dilunga wa Simba akimalizia pasi ya Emmanuel Okwi katika mchezo uliochezwa uwanja wa Uhuru ni bao la usiku kuliko mabao yote msimu uliopita kufungwa ndani ya TPL.
17
Idadi ya asisti za mchezaji wa Yanga, Ibrahimu Ajibu zikiwa ni nyingi kuliko wote msimu uliopita ndani ya TPL, huku akihusika kutupia jumla ya mabao 6 na kufanya kuhusika kwenye jumla ya mabao 23 ya Yanga ambayo imemaliza ligi ikiwa nafasi ya pili na imepachika jumla ya mabao 56.
20
Mchezo wa kwanza kwa Yanga kupoteza mbele ya Stand United uwanja wa Kambarage, Shinyanga, bao lilifungwa na nahodha wa kikosi hicho Jacob Massawe dakika ya 88.
00:53
Bao la mapema kuliko yote msimu uliopita ndani ya ligi kuu lilifungwa na mshambuliaji wa Mtibwa Sugar, Kelvin Sabato sekunde ya 53 kwenye ushindi wa mabao 4-0 uwanja wa Manungu mkoani Morogoro.
212.
Jumla ya sare kwenye Ligi Kuu Bara msimu huu iliyokuwa na timu 38 zilizocheza jumla ya michezo 270 na kukusanya jumla ya mabao 1,028 msimu huu kwenye ligi kuu bara.
4.
Idadi ya michezo ambayo ni michache kushinda kwa timu ya ligi ambayo ni African Lyon katika jumla ya michezo 38 huku kinara akiwa ni Simba ambaye ameshinda jumla ya michezo 29 msimu uliopita.
3.
Idadi ndogo ya michezo ya kupoteza msimu huu ambayo Simba ilipoteza ilikuwa ni mbele ya Mbao FC, Kagera Sugar nje ndani mnyama alipoteza msimu uliopita na timu iliyopoteza michezo mingi kati ya 38 ilikuwa ni African Lyon ilipoteza jumla ya michezo 23 msimu uliopita.
2.
Idadi ya timu zilizoshuka daraja moja kwa moja baada ya kucheza michezo 38, Stand United ilishinda michezo 12, ilipoteza michezo 18 sare 8 na ilifungwa jumla ya mabao 50 huku ikifunga mabao 38 na ilijikusanyia pointi 44.
African Lyon ilijikusanya pointi 23 ilifungwa jumla ya mabao 54 huku safu ya ushambuliaji ikifunga jumla ya mabao 23 na ilimaliza ligi ikiwa na pointi 23.
54.
Mabao mengi kwa utatu wa safu ya ushambuliaji ya Simba iliyo chini ya mshambuliaji Meddie Kagere ambaye amefunga mabao 23, John Bocco mabao 16 Emmanuel Okwi mabao 15.
8
Idadi ya mabao mengi kufungwa timu moja msimu uliopita, Coastal Union ilifungwa mabao hayo mbele ya Simba uwanja wa Uhuru na iliambaulia bao 1 la kufutia machozi.