Home Uncategorized NAMUNGO HAWATAKI UTANI WAANZA NA JEMBE LA ALLIANCE

NAMUNGO HAWATAKI UTANI WAANZA NA JEMBE LA ALLIANCE

UONGOZI wa Namungo FC yenye maskani yake Mtwara imemsajili mshambuliaji wa Alliance FC, Bigirmana Blaise kwa kandarasi ya mwaka mmoja.


Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Namungo, Kidamba Namlia amesema kuwa ni mpango wa mwalimu, Hitimana Thiery kupata wachezaji wenye uzoefu ambao wataipa nguvu safu ya ushambuliaji.

“Mpango uliopo kwa sasa ni kuboresha kikosi chetu, tumeanza na Blaise wengine wanafuata kwani kazi kubwa ambayo tunaifanya ni kusajili wachezaji wenye uzoefu watakosaidia kuleta ushindani msimu ujao.

“Hatutaki wachezaji wa majaribio ama wale ambao uwezo wao ni wa kubahatisha hilo hapana ni lazima tujipange hasa ukizingatia ligi kuu sio sawa na ligi daraja la kwanza,” amesema Namlia.
SOMA NA HII  LICHA YA KIPIGO MALENGO YA TAIFA STARS YAKO PALEPALE KOMBE LA DUNIA