Home Uncategorized NIYONZIMA APEWA SOMO NA SAMAKIBA

NIYONZIMA APEWA SOMO NA SAMAKIBA

KIUNGO fundi wa timu ya Simba Haruna Niyonzima amesema kuwa kitendo walichofanya Mbwana Samatta ambaye ni nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania na Ally Kiba kimempa somo kubwa hivyo atakipeleka Rwanda.

Samatta na Kiba juzi walicheza mchezo wa hisani kupitia taasisi ya Sama Kiba Foundation ukiwa na lengo la kuhakikisha wanarudisha kile wanachokipata kwa jamii inayowazunguka.

Akizungumza na Saleh Jembe, Niyonzima ambaye alikuwa timu Kiba alishuhudia timu yake ikipoteza kwa kufungwa mabao 6-3 amesema kuwa imekuwa ni mara ya kwanza kwake kushiriki ila ni jambo kubwa ambalo limempa soma hivyo ataiga msimu ujao kwa mtindo mwingine.

“Kitendo walichokifanya ni kikubwa na somo kwangu na jamii kiujmla, wakati ujao nami nitafanya hata isipokuwa kwa kucheza nitatumia mbinu nyingine kwani ni kitu kikubwa na chenye thamani.

“Nimekubali kuwa ndani ya timu zote wala sibagui ingawa nipo kwa Kiba na kazi yangu ni mpira hivyo nina imani wakati ujao tutafanya makubwa zaidi kwani wachezaji tuna asili ya kushirikiana,” amesema Niyonzima.

SOMA NA HII  VPL: SIMBA 1-1RUVU SHOOTING