Uncategorized

NYOTA SIMBA KUIBUKIA NAMUNGO

admin June 6, 2019 9:00 pm


IMEBAINIKA kuwa nyota wa Simba, Adam Salamba amekuwa akiwindwa na klabu ya Namungo FC ambayo imepanda daraja pamoja na timu ambayo amewahi kuichezea na Lipuli FC.

Salamba amekuwa akitajwa kuwa ni mchezaji wa simba ambaye Kocha Patrick Aussems hana mpango naye kwa msimu ujao wa ligi na huenda akachwaa au kutolewa kwa mkopo.

Hivyo amekuwa akiwindwa na klabu ya Namungo ambayo ndiyo kwanza imepanda daraja ambayo imeanza mipango yake ya usajili.

Taarifa zinadai kuwa nyota huyo huenda akawa Namungo hata kwa mkopo kama wataafikiana na simba kwa ajili ya msimu ujao.

Gazeti la Spoti Xtra kutoka Global Publishers lilizungumza na mchezaji huyo wa simba, Adam salamba ambaye alifunguka: “Mimi ni mchezaji wa simba hayo unayoyasema sifahamu na sasa bado ni mapema sana mambo ya usajili.”

KOCHA SIMBA KUIBUKIA TIMU NYINGINE LIGI KUU KIPA AGOMEA MKATABA SIMBA / KABWILI SAMATTA MFANO WA KUIGWA – VIDEO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply