Home Uncategorized RASMI SIMBA YAJIONDOA MICHUANO YA KAGAME

RASMI SIMBA YAJIONDOA MICHUANO YA KAGAME


Mabingwa wa Tanzania Bara, Simba SC wamejitoa kwenye michuano ya Kombe la Kagame iliyopangwa kuanza kutimua vumbi Julai mwaka huu nchini Rwanda. 

Akizungumza na Saleh Jembe Mtendaji Mkuu wa Simba Crescentius Magori amesema ni kweli wameamua kujitoa kwenye michuano hiyo huku kutokana na kubwana na ratiba.


“Muda wa maandalizi ya msimu ujao ni finyu kwani kuna baadhi ya wachezaji wako kwenye AFCON na watakaporejea hawatakuwa na muda wa kutosha wa kuwa pamoja na timu.

Amesema mpango wao ni kuweka kambi ya muda usiopungua wiki sita nje ya nchi wakiwa na dhamira ya kufanya vizuri zaidi kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, hivyo ratiba ya Kagame itaingiliana na ratiba ya kambi.


 “Tumepanga kufanya pre-season ya wiki sita kwakuwa tuna lengo la kufanya vizuri zaidi msimu ujao kwenye mashindano ya Kimataifa”, amesema Magori na kuweka bayana kuwa tayari wameshaiandikia barua TFF juu ya uamuzi huo.

SOMA NA HII  NAMUNGO WATUSUA KIMATAIFA,NGOMA UGENINI YAWA 3-3