BAADA ya Simba kuanza kazi na nahodha John Bocco kwa kumpa kandarasi ya miaka miwili sasa imeelezwa kwamba inawasomea rada wachezaji wengine wapya nane ambao mazungumzo yakijibu wanaitwa mezani.
Patrick Aussems, ambaye ni Kocha Mkuu wa Simba ameacha ripoti mezani ambayo imetoa mapendekezo ya kusajili wachezaji wapya nane, kati ya hao watano wawe wa kigeni na watatu wawe wazawa kabla ya kutimika Ubelgji kwa mapumziko.
Sharti lake jepesi alilotoa kwa wachezaji wa kigeni imeelezwa kuwa amesema wawe na uzoefu na michuano ya kimataifa.
Hawa hapa imeelezwa wapo kwenye tageti:-
Yannick Litombo beki wa AS Vita ya Congo.
Ibrahim Saddan kiungo wa KCCA ya Uganda.
Gloudoue Baresi kiraka wa Asec Mimosas ya Ivory Coast.
Rifat Khamis mshambuliaji wa Mtibwa Sugar.
Salum Kihimbwa mshambuliaji wa Mtibwa Sugar.
Emanuel Mvuyekure mshambuliaji wa KMC.
Ramadhan Kapera mshambuliaji wa Kagera Sugar.
David Luhende beki wa Kagera Sugar.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Crescentius Magori amesema kwa sasa Simba haijaanza usajili, muda ukiwadia kila kitu kitawekwa mezani.
“Tulisuka kikosi imara msimu uliopita kwa sasa bado hatujaanza kufanya usajili muda ukifika tutafanya kazi ya kuwapa nafasi wachezaji ambao ni pendekezo la kocha,” amesema.