Home Uncategorized HAYA NDIYO MAMILIONI YALIYOGHARIMU USAJILI WA NYONI, BOCCO NA MANULA SIMBA

HAYA NDIYO MAMILIONI YALIYOGHARIMU USAJILI WA NYONI, BOCCO NA MANULA SIMBA


Mambo ni moto! Hivyo ndivyo unavyoweza kusema baada ya uongozi wa Klabu ya Simba hivi karibuni kuwaongezea mikataba baadhi ya nyota wake kwa ajili ya msimu ujao.

Hata hivyo, wachezaji John Bocco, Erasto Nyoni na Aishi Manula ambao tayari wameongeza mkataba wa kuendelea kuitumikia timu hiyo kwa pamoja usajili wao umeigharimu Simba jumla ya Sh milioni 972.

Habari za kuaminika kutoka ndani ya Simba ambazo Championi Ijumaa imezipata zimedai kuwa wachezaji hao kila mmoja amechukua Sh milioni 100 za usajili.

Kila mwezi kila mmoja atakuwa akilipwa Sh 8,000,000 (milioni nane). Bocco pamoja na Nyoni wao wamesaini mkataba wa miaka miwili, hivyo watalipwa Sh 192m kila mmoja kwa kipindi chote cha mikataba yao, wakati Manula amesaini miaka mitatu, hivyo kwa muda huo wote mshahara wake utaigharimu Simba Sh 288m.

“Ukijumlisha fedha hizo za usajili pamoja na zile za mshahara wao, kwa kipindi chote watakachokuwa na Simba utagundua kuwa wote kwa pamoja watachukua shilingi milioni 972,” kilisema chanzo hicho cha habari.

Alipoulizwa kuhusiana na hilo, Katibu Mkuu wa Simba, Dk Arnold Kashembe, alisema: “Hayo ni mambo ya ndani ya timu, hapaswi kujua mtu yeyote.”

SOMA NA HII  SAKATA LA KICHUYA LAWAPASUA KICHWA NAMUNGO