Uncategorized

HOFU YA NAMUNGO IPO HAPA

admin June 17, 2019 5:03 am


UONGOZI wa Namungo FC umesema kuwa kwa sasa hesabu zao kubwa ni kuona kwamba timu yao inapata nafasi ya kuleta ushindani wa kweli hivyo kazi yao ya kwanza itakuwa ni kujilinda kutokushuka Daraja.

Akizungumza na Salehe Jembe, Kocha Mkuu wa Namungo, Hitimana Thiery amesema kuwa kwa sasa malengo makubwa ya timu ni kucheza soka la kweli litakalowasaidia kutokushuka Daraja.

“Hatari kubwa kwa timu ngeni kwenye ligi ni kushuka daraja, malengo yetu ya kwanza ni kuona tunacheza soka safi, kisha mengine yatafuata.

“Kwa kuligundua hilo tumeanza na mkakati wa kusajili wachezaji makini na wenye uzoefu na nina imani watatusaidia,” amesema.

Namungo FC ni timu yenye maskani yake Lindi, ni miongoni mwa timu 20 ambazo zitashiriki Ligi Kuu Bara msimu ujao.

MFAHAMU MCHEZAJI WA ALGERIA ALIYETUPWA NJE AFCON SABABU YA KUONESHA MAKALI NJE NDANDA FC WAINGIA ANGA ZA YANGA, AZAM FC KUGOMBANIA SAINI YA NYOTA HUYU

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply