Uncategorized

NDANDA FC WAINGIA ANGA ZA YANGA, AZAM FC KUGOMBANIA SAINI YA NYOTA HUYU

admin June 17, 2019 5:23 am


IMEELEZWA kuwa uogozi wa Ndanda FC umeingia kwenye harakati za kuinasa saini ya mshambuliaji wa Mwadui FC, Salum Aiyee kama ilivyo kwa Yanga, ili kuongeza nguvu kwenye kikosi hicho msimu ujao.

Aiyee amekuwa bora kwa msimu wa 2018/19 baada ya kuwakimbiza wazawa wote kwa utupiaji ambapo ametupia jumla ya mabao 18 ambayo ni mara yake ya kwanza kuyafikia tangu aanze kucheza soka la ushindani.

Akizungumza na Salehe Jembe, Aiyee amesema kuwa kwa sasa ametuliza kichwa ili apate timu ambayo itamfaa kwani ofa mkononi mwake ni nyingi.

“Mimi ni mchezaji na msimu uliopita nimepambana kwa ajili ya timu yangu na matokeo yake kwa sasa nina ofa nyingi, wakati ukifika nitasema ni timu ipi nitakwenda,” amesema Aiyee.

Miongoni mwa timu ambazo amekuwa akihusishwa kwenda ni pamoja na Azam FC, Yanga, Alliance, Polisi Tanzania na Singida United.

HOFU YA NAMUNGO IPO HAPA MCHEZAJI AMBAYE HANA UHAKIKA WA KUONGEZEWA MKATABA AIPA YANGA STRAIKA WA SWEDEN

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply