UONGOZI wa Yanga umesema kuwa kwa sasa hauna hesabu za kusajili wachezaji wengine wa kigeni baada ya kukamilisha asilimia 90 za wachezaji waliokuwa wanahitajika na Kocha Mkuu, Mwinyi Zahera.
Mwenyekiti wa Yanga, Dk.Msindo Msolla amesema kuwa kwa sasa hawana mpango wa kugombea wachezaji wa kigeni.
“Tumekamilisha zoezi la usajili kwa wachezaji wa kigeni ambao walikuwa ni pendekezo la Kocha Mwinyi Zahera, hivyo kwa sasa hatuna hesabu za kuongeza wachezaji wa kigeni kwani zoezi limekamilika kilichobaki kwa sasa ni kuwatambulisha,” amesema.