Home Uncategorized AKIWA HAJAMALIZA HATA WIKI, BALINYA ATUMA MJUMBE MZITO KWA WACHEZAJI BONGO

AKIWA HAJAMALIZA HATA WIKI, BALINYA ATUMA MJUMBE MZITO KWA WACHEZAJI BONGO


NYOTA mpya wa klabu ya Yanga, mshambuliaji Juma Balinya amefunguka kwamba kwake hawazi sana nani ambaye ataanza naye kwenye pacha ya ushambuliaji ya timu hiyo, kwani anaamini atashirikiana naye vizuri na kuifanya kazi yake ya kufunga.

Balinya aliyefunga mabao 19 kwenye Ligi Kuu ya Uganda msimu uliopita, ametua Yanga kwa mkataba wa miaka miwili ambapo alitangazwa Jumamosi iliyopita.

Balinya kwa msimu ujao kwenye pacha ya klabu hiyo anaweza kucheza na straika mmoja kati ya Mnamibia Sadney Urithob au Maybin Kalengo ambao nao wamesajiliwa msimu huu.

Akizungumza na Championi Jumatano, Balinya amesema kwake haangalii ni aina gani ya mchezaji ambaye atapangiwa kucheza naye badala yake amejipanga kushirikiana na mchezaji yeyote katika kuifungia mabao timu hiyo.

“Hapa mimi ni mgeni na simfahamu mchezaji yeyote yule ambaye nitachezeshwa naye kwenye kikosi cha kwanza.

“Lakini hilo kwangu siyo shida sana kwa sababu nimejipanga kuifanya kazi yangu vizuri, nitakayepangiwa naye mimi nitashirikiana naye katika kuifungia timu na kuhakikisha inapata matokeo yaliyo mazuri.

“Nikishakaa kwa muda kidogo nitazoeana na wenzangu, ambapo hapo tutafanya vizuri zaidi,” alisema Balinya.

SOMA NA HII  MEDDIE KAGERE AMJIBU KIBABE BOSSI WAKE SVEN