Uncategorized

ALLIANCE FC WATANGAZA HATMA YA KOCHA WAO MALALE HAMSINI

admin June 20, 2019 1:02 pm


UONGOZI wa Alliance FC umesema kuwa kwa sasa wanamsubiri kocha wao Malale Hamsini asaini kandarasi mpya ili aendelee na kazi kwani msimu uliopita alifanya mambo makubwa.

Kwa sasa Hamsini amemaliza mkataba wake na bado hajasaini mkataba mpya kwa kile alichodai kwamba bado hajawasiliana na viongozi wa Alliance FC.

Akizungumza na Salehe Jembe, Ofisa Habari wa Alliance, Jacson Mwafulango amesema kuwa wanaamini uwezo wa Hamsini hali iliyofanya wamuandalie mkataba mapema.

“Sisi Alliance tunatambua kwamba Hamsini ni kocha wetu ndio mana tumemuandalia mkataba hivyo kilichobaki kwa sasa ni yeye mwenyewe kusaini ili kuendeleza mipango kwa ajili ya msimu ujao,” amesema.

AZAM FC WAIKOMALIA KAGAME, SASA NGUVU ZAO WAMEWEKEZA HUKU JEZI ZA STARS ZAGOMBEWA KAMA NJUNGU, WADAU WAJITOKEZA KUISAPOTI IFANYE KWELI AFCON

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply