Home Uncategorized MZEE AKILIMALI ATOA TAMKO JUU YA ROSTAM AZIZ, AUNGANA NAYE

MZEE AKILIMALI ATOA TAMKO JUU YA ROSTAM AZIZ, AUNGANA NAYE


Mjumbe wa Baraza la Wazee Yanga, Mzee Ibrahim Akilimali โ€˜Mzee Akilimaliโ€™ ambaye ni Katibu ameunga mkono hoja ya Rostam na kusema Yanga haiwezi kumilikiwa na mtu mmoja.

โ€œKwa kweli mimi nimefurahishwa na kauli ya Rostam na ninamkubali sana kwani klabu kubwa kama Yanga ambayo ina wanachama wengi huwezi kuimilikisha na mtu mmoja kwani kufanya hivyo ina maana kila kitu atakuwa nacho yeye.

โ€œMimi jana nilimsikiliza mwenyewe na timu kama Yanga inatakiwa iongozwe na wanachama sasa kama mwanachama umeenda pale na kudhani kuwa kuna mdhamini uache kuchangia basi wewe hufahi kuwa mwanachama, mwanachama unatakiwa uchangie.”

Kauli ya Akilimali imekuja mara baada ya Rostam kuibuka na kusema anataka kuifadhili Yanga kupitia makampuni yake na si kuimiliki.

SOMA NA HII  CHEKI MOTO WA KIKOSI BORA CHA WIKI CHA SIMBA NA YANGA