Timu YA SOKA YA Taifa Ya Tanzania ‘Taifa Stars’ inataraji kucheza mchezo wake wa kwanza wa hatua ya makundi katika fainali za kombe la Mataifa ya Afrika dhidi ya Senegal ‘Simba wa Teranga’ katika dimba la Juni 30 huko nchini Misri huku nyuma kukiwa na madai ya uwepo wa mgomo wa wachezaji jana Jumamosi wakishinikiza kulipwa stahiki zao.
Stars inacheza michuano hii kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1980 ilipofuzu kwa mara ya kwanza katika fainali zilizofanyika nchini Nigeria. Kikosi hicho ambacho kinanolewa na mshindi wa michuano hiyo kiuchezaji, gwiji wa Nigeria, Emmanuel Amunike kinaingia kucheza majira ya saa mbili kwa saa za Afrika Mashariki kuikabili Senegal ambao licha ya kuwahi kufika fainali mara mbili miaka 1992 na 2002, pia timu hiyo kutoka Magharibi mwa Afrika wana uzoefu wa kutosha- wakicheza fainali hizi mara 12.
CHA KUFANYA
Tayari tumeona michezo minne ikichezwa kuanzia usiku wa Ijumaa- michezo miwili ya kundi la kwanza ( Misri 1-0 Zimbabwe, DR Congo 0-2 Uganda) na michezo mingine miwili ya kundi la pili ( Nigeria 1-0 Burundi, Guinnea 2-2 Madagacsar) ambayo kimsingi imezalisha magoli nane ( wastani wa magoli mawili kwa kila mchezo)
Senegal haitakuwa na staa wao mkubwa Zaidi katika kikosi mshambulizi Saido Mane lakini bado kuna nafasi kubwa ya Simba hao wa milima ya Teranga ‘kuichanachana’ Stars kwa kutumia washambuliaji wawili, Mbaye Niang sambamba na pacha mwenzake katika kikosi cha Rennes ya Ufaransa, Ismaïla Sarr .
Kiungo mshambulizi wa Inter Milan, Keita Baldé huyu atakuwa changamoto kubwa kwa mlinzi wa kulia wa Stars, Hassan Kessy. Akiwa na miaka 20 hivi sasa kiungo wa kulia wa klabu ya Club Brugge, Krépin Diatta atakuwa winga wa kulia na upande huu anaweza kukutana na mlinzi Gadiel Michael.
Washambuliaji hao wane wanapaswa kukabwa kwa umakini mkubwa kwa sababu licha ya uzoefu wa timu yao katika michuano, wao wenyewe tayari wamejidhihirisha ni wachezaji wa kiwango cha juu. Uchezaji wa walinzi wa kati, Kelvin Yondan, Ally Mtoni/David Mwantika unatakiwa kuwa wa tahadhari mno kwa sababu kosa lolote linaqweza kuwapatia galo/magoli ama mikwaju iliyofuka- penalty na faulo za karibu na lango.
Hii si mechi ya kushambulia hata kidogo kwa walinzi wa Stars na kama ningepata nafasi ya kutoa ushauri kwa kocha Amunike ningemshauri aanze nan a walinzi watano katika ngome- watatu ( Dav, Kelvin na Ally) na walinzi katika fullbacks ( Kessy na Gadiel) ili kujaribu kuwa salama.
Senegal watashinda mchezo huu kutokana na maandalizi yao sambamba na aina ya vikosi vinavyokutana, lakini Stars haipaswi kupoteza kwa idadi kubwa ya magoli ( 1-0) si mbaya lakini kuanzia tofauti ya magoli mawili ni tatizo.
Nidhamu ya kujilinda inapaswa kuwa juu hasa kwa Kelvin na Sonso ambao wamekuwa na kawaida ya kucheza kwa nguvu kuliko bila ya kutazama maeneo na wakati wa kutumia nguvu Zaidi.kuzuia ndio silaha ya kwanza hivyo Stars inapaswa kuwazuia wane hawa wenye njaa japo halitakuwa jambo rahisi.
KUMILIKI MPIRA….
Himid Mao, Feisal Salum, na Mudathir Yahya wanaweza kuwa msaada mkubwa katika eneo la kati wanaweza kuibana Senegal katika eneo la kati kutokana na kwamba kikosi cha Alou Cisse kinapendelea kucheza mchezo wa 4-4-2 ambapo kati mwa uwanja hupangwa, Gueye na Ndiaye.
Stars inapaswa kuhakikisha wanazuia na kumiliki mpira na inaweza kuwa vizuri Zaidi kwa sababu Stars ina washambuliaji wawili wenye kasi, Mbwana Samatta na Saimon Msuva. Katika mfumo wa 5-3-2 Stars inaweza kuhimili nguvu ya Simba wa Teranga, nje yah apo sioni njia ya kuepeka kichapo.
KUSHAMBULIA….
Kumchezesha Msuva kama mshambulizi wa kwanza, Samatta akicheza nyuma yake itawapa walinzi wa Senegal wakati mgumu kiasi na kuwafanya wasiende sana kushambulia goli mwa Stars. Mlinzi wa Schalke 04, Salif Sane na yule wa SS Napoli, Kalidou Koulibaly ndio nguzo ya safu ya ulinzi ya Senegal katika beki ya kati hivyo inaweza kuonekana ni kiasi gani kuna changamoto kwa Stars kupata goli/magoli.
Mlinzi wa FC Barcelona, Moussa Wagué katika beki ya kulia, na yule wa Orlando City ya Marekani , Lamine Sané( kaka wa Salif) wanaunda ukuta wa walinzi wan ne wa kikosi cha Cisse na wote wana ubora mkubwa. Stars inapaswa kushambulia vizuri kwa kasi, hasa mashambulizi ya kushtukiza kupitia Msuva na Samatta.
The post Ni 5-3-2 pekee itakayo ‘inusuru’ Stars na ‘dhoruba’ la Senegal appeared first on Kandanda.