Home Uncategorized AZAM YAITANGAZIA VITA SIMBA, WACHEZAJI WATAJWA

AZAM YAITANGAZIA VITA SIMBA, WACHEZAJI WATAJWA


Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin ‘Popat’, amesema kuwa msimu ujao wa Ligi Kuu Bara wataivua ubingwa Simba.

Azam FC ambayo msimu uliopita ilishika nafasi ya tatu huku ikitwaa ubingwa wa Kombe la Shirikisho kwa kuifunga Lipuli FC, imepania kufanya kweli msimu ujao kwa kulitwaa taji la Ligi Kuu Bara linaloshikiliwa na Simba kwa msimu wa pili mfululizo sasa.

Popat aliyasema hayo jana Alhamisi alipotembelea ofisi za gazeti hili zilizopo kwenye Jengo la Global Group, Sinza Mori jijini Dar na kufanya mahojiano na +255 Global Radio katika kipindi maalumu cha michezo.

“Msimu ujao ubingwa ni wa kwetu hilo halina ubishi, tumechoka kuwa wasindikizaji, sasa imefika zamu yetu ya sisi kuwa mabingwa tena wa Ligi Kuu Tanzania Bara,” alisema Popat.

Popat aligusia pia suala la wachezaji waliotemwa na kufunguka kuwa: “Wale wachezaji walikatwa na kocha mpya Etienne Ndayiraije, hivyo sisi kama uongozi hatukuwa na kipangamizi juu ya maamuzi hayo.”

Azam FC wameanza mazoezi baada ya wachezaji kuwasili juzi klabuni na sasa wanajiandaa na safari ya kwenda Rwanda kushiriki mashindano ya Kagame Cup. 

SOMA NA HII  MAGANGA ALIVYOTAMBA KUIDHALILISHA SIMBA KWA MKAPA - VIDEO