Home Uncategorized KOTEI MWENYEWE AFUNGUKA JUU YA KWENDA YANGA

KOTEI MWENYEWE AFUNGUKA JUU YA KWENDA YANGA


Kiungo mkabaji ambaye mkataba wake umemalizika na klabu ya Simba, Mgahana, James Kotei amesema haelewi juu ya hatma yake ndani ya kikosi hicho kutokana na kutopata mawasiliano na kiongozi yeyote wa Simba juu ya kuhitajika kwa msimu ujao.

“Kwa sasa mimi nipo mapumziko tu huku nyumbani, ninacheza na watoto na familia yangu kiujumla sifahamu lolote juu ya usajili wangu.

“Hadi sasa sijapata simu yoyote ile kutoka kwa kiongozi yeyote wa Simba jambo ambalo linanifanya nisielewe juu ya suala la kurudi kwa msimu ujao, labda tuendelee kusubiri kuona inakuwaje hadi siku za mapumziko zitakapoisha,” alisema Kotei.

KUHUSU YANGA

Kotei amesema yupo tayari kwenda popote kwa ajili ya kusaka maisha kwani mpira ndiyo unaomfanya apate anachokitaka.

“Ninaweza kwenda kokote kule kwa sababu ninataka niwe nacheza tu, siyo Yanga pekee hata klabu nyingine yoyote ile.

“Kama itakuwa hivi kwa Simba kukaa kimya ninaweza kwenda kwingine kokote ambapo mawakala wangu watakuwa wananitafutia. Lakini kitu kikubwa zaidi mimi ninataka kucheza ili nilinde kipaji changu.”

SOMA NA HII  ZIDANE ANA MAMBO MANNE YA KUWEKA SAWA REAL