Home Uncategorized GADIEL AWATUMIA UJUMBE WA KIBABE KENYA, WALA HANA HOFU

GADIEL AWATUMIA UJUMBE WA KIBABE KENYA, WALA HANA HOFU


BEKI wa kushoto wa Taifa Stars, Gadiel Michael, amewaondoa shaka Watanzania na kuahidi kupambana kufa na kupona katika mchezo wa leo Alhamisi dhidi ya Kenya.

Taifa Stars na Kenya, kesho zitapambana kwenye michuano ya Kombe la Mataifa Afrika (Afcon), ukiwa ni mchezo wa Kundi C, ambapo katika mechi zao za kwanza, zote zilifungwa kwa idadi sawa ya mabao. Taifa Stars ilifungwa na Senegal, Kenya ikafungwa na Algeria.

Gadiel amesema, kwenye mchezo wa leo dhidi ya Kenya watapambana kupata ushindi kwa kuwa wanawafahamu wapinzani wao na kupata ushindi kwenye mchezo huo kutatoa mwanga wa wapi wanakwenda katika mashindano ya Afcon.

“Mechi na Kenya naamini ndiyo itakayotupa sisi pointi na kupata mwanga wa kwenda mbele zaidi katika mashindano haya, nafahamu mchezo utakuwa mgumu kwa kuwa sisi wote tulipoteza kwenye michezo ya kwanza.

“Sisi kama wachezaji tumejipanga na tunawajua wale ni majirani zetu hakuna kitakachoshindikana, kitu pekee tulichopanga wachezaji ni kupambana kufa na kupona kama tutapoteza itakuwa mbaya kwetu na Watanzania kwa ujumla,” alisema Gadiel.

SOMA NA HII  MAURIZIO SARRI KIBOKO KWA SIKU ANAVUTA 'MISIGARA' KIBAO