Home Uncategorized LUKAKU ANAONDOKA ZAKE MAN UNITED

LUKAKU ANAONDOKA ZAKE MAN UNITED


Imeripotiwa kuwa Romelu Lukaku ameamua kuondoka Manchester United, hii ni kwa mujibu wa wakala wake.

Straika huyo mwenye umri wa miaka 26 anatazamiwa kuachana na timu hiyo na uwezekano mkubwa ni kuwa atajiunga na Inter Milan msimu ujao wa 2019/20.

Wakala wa Lukaku Federico Pastorello amesema kuwa staa wake amemweleza kuwa anataka kuondoka katika timu hiyo.

Pastorello alidokeza kuwa Inter Milan ipo kwenye jitihada za kumalizana na Manchester United ili Lukaku aende Inter Milan.

“Lukaku ana ndoto zake za soka, na ameweka wazi kuwa anataka kuondoka ili aende Inter Milan,” alisema Pastorello juzi baada ya kukutana na viongozi wa Inter jijini Milan.

Alisema Inter Milan ipo kwenye harakati za kukamilisha usajili wa straika huyo wa timu ya taifa ya Ubelgiji. Lukaku amekuwa na wakati mgumu katika kikosi cha Manchester United kiasi cha kupoteza namba.

Lukaku alipachika mabao 15 msimu wa 2018/19 ambao alijikuta akipoteza namba kwa Marcus Rashford.

Amekuwa na wakati mgumu huku akilaumiwa kwa kushindwa kuonyesha thamani yake baada ya kununuliwa kwa dau la pauni milioni 75 (Sh. bilioni 218) kutoka Everton mwaka 2017.

Mara ya kwanza kocha Ole Gunnar Solskjaer alikuwa na imani kubwa na Rashford lakini bahati mbaya straika huyo alishindwa kuonyesha makali yake uwanjani.

Lukaku inasemekana alishafikia muafaka wa masuala ya mishahara na Inter Milan, ambapo suala lililobakia ni kwa Inter Milan na Manchester United, Manchester United imeshikilia kumuuza kwa pauni milioni 75 (Sh. bilioni 218) ambazo ilimnunua kutoka Everton, ambapo Inter imegomea bei hiyo.

SOMA NA HII  BERNARD MORRISON APEWA ONYO - VIDEO