Home Uncategorized YANGA YAKAMILISHA FASTA USAJILI CAF

YANGA YAKAMILISHA FASTA USAJILI CAF


MABOSI wa Yanga wapo kwenye dakika za mwisho za kukamilisha usajili wao wa msimu ujao kwa ajili ya kuwahi dirisha la usajili la Shirikisho la Soka Afrika (Caf) ambalo linafungwa Jumapili, Juni 30.

Yanga washamalizana na wachezaji 10 ambao wataanza kuwatumia msimu ujao. Baadhi ya wachezaji ambao wamesajiliwa na Yanga ni Juma Balinya, Abdulaziz Makame, Ally Ally, Balama Mapinduzi na Lamine Moro. Issa Bigirimana, Patrick Sibomana, Lamine Moro, Sadney Urithob na Maybin Kalengo.

Mwakalebela amesema: “Usajili wetu umekamilika kilichobaki kwa sasa ni kumalizia sehemu ambazo tunaona zinahitajika kufanyika hivyo.

“Tunawahi kusajili mapema ili tuwahi dirisha la Caf ambalo linafungwa Juni 30. Kwa hiyo tutakachofanya ni kusajili majina tutatuma huko.

SOMA NA HII  KARIAKOO DABI,SIMBA QUEENS V YANGA PRINCESS VITA YA KUTIBUA REKODI