Home Uncategorized MASTAA YANGA WAANZA KUTUA AIRPORT

MASTAA YANGA WAANZA KUTUA AIRPORT


WACHEZAJI wapya wa Yanga na wale wa zamani wanatarajia kuanza kuingia nchini wiki hii kwa ajili ya kujiandaa na kambi ya timu hiyo inayotarajiwa kuanza rasmi Julai 7, mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Tayari Yanga imeshasajili nyota 10 wapya wakiwemo wazawa ambao ni Mapinduzi Balama, Abdulaziz Makame,Ally Ally, kwa upande wa wageni ni Patrick Sibomana, Sadney Urikhob, Issa Bigirimana ‘Wacott’, Maybin Kalengo, Juma Balinya, Lamine Moro na Suleiman Mustapha.

Mratibu wa kikosi hicho Hafidh Saleh alisema, wanatarajia kuingia kambini Julai 7 mwaka huu hivyo kwa kuwa hawatakuwa na muda wa kuchelewesha ‘programu’ wachezaji wale waliopo nje ya nchi wanatakiwa kuanza kuingia kwenye Uwanja wa Ndege nchini kuanzia mwishoni mwa wiki hii.

“Tunatarajia kuanza maandalizi mapema maana mbele yetu tutakuwa na mchezo wa kirafiki siku ya kilele cha tamasha letu la Mwananchi, ambapo pia siku hiyo itatumika kuwatambulisha nyota wapya na kikosi chote kwa ujumla kama ilivyotangazwa hivi karibuni pale Diamond Jubilee.

“Sina taarifa rasmi kama kambi itakua nchi gani zaidi nafahamu maandalizi ya awali yatafanyikia hapahapa kwa zaidi ya wiki mbili nadhani baada ya hapo kocha ndiyo atatoa muongozo wake na mahali gani tutahamishia kambi mapema kabla ya msimu mpya kuanza,” alisema Hafidh.

SOMA NA HII  EYMAEL WA YANGA AZIPIGIA HESABU POINTI TATU ZA RUVU SHOOTING NAMNA HII