TARAJIA kuiona Yanga bab kubwa kwenye msimu ujao wa Ligi Kuu Bara, ni baada ya jana jioni bosi mpya wa usajili kupanda ndege na kwenda nchini Misri kwa ajili ya kukamilisha usajili wa wachezaji wanne wa Timu ya taifa, Taifa Stars.
Yanga hivi sasa ipo kwenye mipango thabiti ya kukiimarisha kikosi chao kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Bara ambayo hadi hivi sasa tayari imekamilisha usajili wa wachezaji tisa pekee ambao ni Abdulaziz Makame na Mapinduzi Balama.
Wengine ni Ally Ally, Issa Bigirimana ‘Walcott’, Patrick Sibomana, Sadney Urikhob, Maybin Kalengo, Juma Balinya, Lamine Moro na Suleiman Mustapha.
Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Spoti Xtra, bosi huyo jana jioni alitarajiwa kupanda ndege kuelekea Misri ilipo Stars kwenye michuano ya Kombe la Mataifa Afrika Afcon.
Mtoa taarifa aliwataja wachezaji hao wanne ni makipa, Farouk Shikhalo anayeichezea Bandari ya Kenya na kipa wa Azam FC aliyekuwa anacheza kwa mkopo Mbao FC, Metacha Mnata.
Aliwataja wengine ni mabeki, Gadiel Michael aliyemaliza mkataba wake wa kuichezea timu hiyo na beki kiraka wa Lipuli FC, Ally Mtoni ‘Sonso’, anayemudu kucheza beki wa pembeni kushoto na kati.
“Mwenyekiti wetu wa usajili (Frank Kamugisha) leo jioni anatarajiwa kupanda ndege kwenda nchini Misri ilipokuwa timu ya taifa, Taifa Stars kwa ajili ya kukamilisha usajili wa wachezaji wanne ambao wote wazawa.
“Bosi huyo anakwenda huko baada ya kufikia muafaka mzuri na mameneja wanaowamiliki wachezaji hao, hivyo mara baada ya kutua huko atakamilisha usajili wao kwa kuwasainisha mikataba ya miaka miwili kila mmoja.
“Wachezaji hao wanasajiliwa kwa mujibu wa ripoti ya kocha aliyoitoa kwa uongozi kuwa ni lazima wachezaji hao wasajiliwe katika kukiimarisha kikosi chao kinachojiandaa na Ligi ya Mabingwa Afrika na Ligi Kuu Tanzania Bara,”alisema mtoa taarifa huyo.
MASHINE ZINGINE AFCON KUMALIZANA NA YANGA, BOSI ASAFIRI
SOMA NA HII ALIKIBA AUNGANA NA CHUMA ' MEDDIE KAGERE' KUMMALIZA SAMATTA LEO, TAZAMA TIZI LAO - VIDEO