Home Uncategorized MONDI AMPA MSALA KIBA!

MONDI AMPA MSALA KIBA!


DAR ES SALAAM: Weka pembeni nyimbo zake za mwaka huu za Tetema, The One na Inama, sasa ni zamu ya Kanyaga kutoka kwa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ambao umesababisha kizazaa kwa hasimu wake kimuziki, Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’, Amani linafunguka. 

Mapema wiki hii, Diamond au Mondi aliachia wimbo huo ambao hadi juzi Jumanne mchana ulikuwa na watazamaji zaidi ya laki mbili kwenye Mtandao wa YouTube ndani ya siku moja. Wimbo wa Kanyaga umebeba maudhui mengi na neno “kanyaga” limetumika kama kuachana na kitu au kupotezea jambo.

MSALA KWA KIBA

Mapokezi ya wimbo huo ndiyo yaliyozaa msala kwa Kiba ambaye baadhi ya mashabiki walidai kuwa hawapi kile wanachokifanya badala yake wanalazimika kusikiliza wimbo huo mpya wa Mondi.

“Kiukweli Kiba unavyotutenda sisi fans (mashabiki) wako siyo sawa. ‘UNATUVUA NGUO’ “Hatuna nyimbo zako za kujidai nazo mpaka tunacheza nyimbo za huyu jamaa (Mondi). Haki unatuvua nguo mashabiki wako. Hebu ona mashabiki wako tunavyotia aibu! “Haki ya nani hebu achana na kulea bwana, tuliza akili, toa nyimbo za maana.

“Unajua Kiba unanyamaza sana siku hizi mpaka jina lako la mfalme (King Kiba) utanyang’anywa maana kwa sasa humkuti Diamond hata robo. “Haki mjue nilikuwa ninacheza huku ninalia kindanindani. Nacheza huku naumia roho kucheza wimbo huu wa Diamond.

“Nimejikuta tu kwani sasa nitafanyaje? Kiba siku hizi nyimbo zake hazieleweki. Bora hata zamani alivyokuwa anakakaa kimya muda mrefu halafu akiibuka, anaibuka na dude. “Hizi nyimbo zake anazotoa siku hizi zinamshushia status (heshima). “Nasema hivi siyo kwa ubaya, lakini ni kwa upendo nilionao kwa Kiba.

‘ANGALAU NANDY’

“Kiukweli Kiba tumechoka, Januari hadi Desemba tunamsikiliza tu Diamond na wanaye tu, angalau kidogo Nandy (staa wa kike wa Bongo Fleva, Faustina Charles Mfinanga) analeta ushindani.

“Tumechoka bwana, Kiba hebu achana na ulezi bwana, kwa nini hutoi muziki wa maana? “Inabidi tu tumsikilize Diamond maana Kiba hatujali sisi fans wake…” ilisomeka sehemu ya maoni mengi kwenye mitandao ya kijamii baada ya Mondi kuachia wimbo huo wa Kanyaga na kugeuka gumzo kila kona huku akiendelea kugandwa na ile skendo ya Freemason inayohusishwa na lebo yake ya Wasafi Classic Baby (WCB) kuwa ndiyo chanzo cha mafanikio yake.

NYIMBO ZA KIBA

Kwa mwaka huu, Kiba ameachia wimbo mmoja wa Mbio na mwingine alishirikiana na Ommy Dimpoz, Cheed -Rockstar! Katika mahojiano na Gazeti la Amani, Mondi alifunguka juu ya wimbo huo na kwamba kwa sasa yupo kikazi zaidi baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu akijihusisha na projekti nyingine.

“Nafurahi kusikia Wimbo wa Kanyaga unafanya vizuri mno. “Ni kweli nilikuwa kimya kwa muda mrefu bila kuachia wimbo, lakini sasa hivi ni hit after hit (wimbo baada ya wimbo). “Nilikuwa na projects nyingine ikiwemo kuimarisha media zangu na ndiyo maana sikutoa ngoma kwa ajili ya tuzo.

“Sasa nimerudi rasmi hivyo mashabiki wangu watarajie kazi nzuri yaani ni bandika bandua,” alisema Diamond. Alipotafutwa Kiba ili kujua mipango yake na kufikishiwa malalamiko ya mashabiki wake hakupatikana hewani huku watu wake wa karibuni wakisema yupo Ulaya kwa ajili ya shoo.

MONDI NA KIBA

Kwa muda mrefu Mondi na Kiba wamekuwa wakisababisha mgawanyiko wa mashabiki huku kila upande ukiamini wenyewe ndiyo bora kuliko mwingin.

SOMA NA HII  AZAM YAMFUATA MRITHI HUYU WA DAVID KISSU