MENEJA wa Ibrahimu Ajibu, Athuman Ajibu amesema kuwa timu atakayojiunga mteja wake itajulikana.
Ajibu alikuwa anatakiwa kujiunga na TP Mazembe dili hilo liliyeyuka kwa kile kilichoelezwa dau kubwa huku akitajwa tayari amemalizana na Simba.
Akizungumza na Saleh Jembe, Ajibu amesema kuwa kwa sasa mambo bado ni magumu kwake hivyo mpaka jioni atakuwa amemaliza kazi.
“Kwa sasa mambo bado hayajawa sawa, itafahamika leo timu ambayo atajiunga kwani kuna vitu ambavyo ilikuwa bado havijakamilika, kuhusu Mazembe hiyo ishabuma,” amesema Ajibu.