Home Uncategorized POGBA ATAKA KUSEPA MANCHESTER UNITED MAZIMA

POGBA ATAKA KUSEPA MANCHESTER UNITED MAZIMA


PAUL Pogba, kiungo mshambuliaji wa Manchester United amesema kuwa itakuwa habari njema kwake kuondoka ndani ya kikosi hicho ili kupata changamoto mpya mbali na Premier League.
Mfarasa huyo anahusishwa kujiunga na Real Madrid ili kufanya kazi na meneja Zinedine Zidane ama kurejea kwenye kikosi chake cha zamani cha Juventus.
Pogba akiwa ndani ya United amekuwa akilaumiwa na mashabiki kwa kucheza chini ya kiwango akiwa ndani ya uwanja.
“Kuna mambo mengi ambayo yanazungumzwa juu yangu kwa sasa na wengi ambao wanafikiria juu yangu naamini ni mambo mazuri.
“Kwangu mimi nimekuwa ndani ya Manchester United kwa muda wa miaka mitatu na nimefanya mengi makubwa, nimekuwa na vipindi vizuri na vibaya pia kama ilivyo kwa wengine, hilo ni jambo la kawaida popote pale.
“Baada ya msimu huu na kila kitu ambacho kimetokea ndani ya msimu huu, nina amini ulikuwa ni msimu bora kwangu, kwa sasa nadhani itakuwa ni muda mzuri kwangu kupata changamoto mpya sehemu nyingine,” amesema.

SOMA NA HII  KMC WAANZA KUIVUTIA KASI COASTAL UNION, WACHEZAJI LEO KULA BATA