Home Uncategorized BEKI MPYA YANGA ATUMA UJUMBE MZITO KWA WAPINZANI

BEKI MPYA YANGA ATUMA UJUMBE MZITO KWA WAPINZANI


BEKI mpya wa Yanga ambaye kwa sasa yupo na timu ya Taifa nchini Misri, Ally Mtoni ‘Sonso’ amesema kuwa ana imani ya kufanya makubwa msimu ujao ndani ya kikosi chake kipya.

Sonso amesema kuwa kwa namna anavyomtambua beki mkongwe Kelvin Yondani itakuwa ngumu kwa wapinzani kupita ukuta wa Yanga.

“Natambua uwezo wa Yondani ndani ya Yanga, hivyo uwepo wangu ndani ya kikosi utafanya tuwe na kikosi kipana na itakuwa ngumu kwa washambuliaji kupita ukuta wetu, hivyo ni jambo la kusubiri na kuona,” amesema Soso ambaye amejiunga na Yanga akitokea Lipuli.

SOMA NA HII  VIDEO: YATAZAME MABAO SITA YALIYOPATIKANA MCHEZO WA SIMBA V ALLIANCE