Uncategorized

YANGA KUJA KIVINGINE WAKATI WA USAJILI, MFUMO MPYA KUTUMIKA

admin April 13, 2020 8:27 am

UONGOZI wa Yanga umesema kuwa utatumia mfumo mpya wa kufanya usajili wa wachezaji wao ili kupata wachezaji watakaoleta ushindani ndani ya kikosi chao msimu ujao.

Kwa sasa Ligi Kuu Tanzania Bara imesimama kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona ambapo wachezaji wengi wapo nyumbani wakifanya mazoezi binafsi.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa watafanya mambo kipekee ndani ya msimu huu katika kuboresha kikosi chao.

“Tupo vizuri kwa sasa na tunaamini kwamba wakati ukifika tutaleta upekee wa katika mfumo wa usajili wa wachezaji wetu na mfumo utakuwa ni wa kipekee kuepuka zile janjajanja ambazo zimezoeleka.

“Kikubwa kwa sasa mashabiki watulie wasiwe na presha kila kitu kipo sawa na mambo yatakuwa vizuri wenyewe watapenda ila wasisahau pia kuchukua tahadhari ya Virusi vya Corona,” amesema.

NYOTA KANE ANAWINDWA NA MANCHESTER UNITED BRUNO TARIMO AJIPA UBALOZI NCHINI SERBIA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply