Uncategorized

OKWI ABWAGA MANYANGA SIMBA, ATIMKIA UARABUNI

admin July 10, 2019 9:43 am


IMEELEZWA kuwa nyota wa Simba Emmanuel Okwi amejiunga na timu ya Fujairah Footbal Club inayoshiriki Ligi Kuu Uarabuni.

Okwi ambaye msimu wa 2018-19 akiwa ndani ya Simba alifunga jumla ya mabao 15 na anashikilia rekodi ya kufunga ‘hat trick’ nyingi kuliko wote akifunga jumla ya mbili ameshindwa kuelewana na mabosi zake Simba.

Imeelezwa kuwa miongoni mwa timu ambazo zilikuwa zinahitaji huduma yake ni pamoja na Simba ambao walishindwana naye kwa dau alilohitaji kuwekewa mezani huku klabu nyingine ambazo ni pamoja na Kaizer Chief ilitajwa kuwa miongoni mwa timu iliyokuwa inahitaji saini yake.

MGANGA HUKO BENIN AMTAKA MANE KUTOCHEZA MECHI YA LEO ILI KUEPUKA KIFO BIASHARA UNITED YAFANYA BIASHARA NA AMRI SAID

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply