Uncategorized

JOSE MOURINHO ASAKA TIMU YA KUFUNDISHA ADAI ANA HASIRA NA KAZI

admin July 14, 2019 1:35 pm
JOSE Mourinho kwa sasa anafikiria kurejea kwenye benchi la ufundi akiwa ni meneja endapo atapata timu sahihi.
Mourinho mwenye miaka 56 amekuwa bila timu kwa muda mrefu baada ya kupigwa chini ndani ya kikosi cha Manchester United, Desemba mwaka jana.
Amekuwa akihusishwa kujiunga na timu ya Benfica msimu ujao, Lyon na Newcastle United wametajwa kumhitaji bosi huyo ambaye ameinoa pia Chelsea na Real Madrid.
“Mpango wangu kurejea kazini upo na nina hasira ya kazi ila kwa sasa ninasubiri timu sahihi ambayo nitaifundisha nikiwa na mipango sahihi.
“Wakati sahihi ukifika nitafanya mambo ambayo nimewahi kuyafanya ninapenda kazi na ninapenda pia michezo mingine mbali na mpira naona kwa sasa ni muda wangu wa kufurahia,” amesema.
TAMBWE AMEMTUMIA UJUMBE HUU ZAHERA KUHUSIANA NA YONDANI KOCHA MPYA YANGA AANZA KAZI NA KINDOKI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6131

Leave a Reply