Deogratius Munish, mlinda mlango huru baada ya kuachana na Simba amesema kuwa ana ofa tano mkononi mwake kwa sasa.
Dida hana timu na anatumia muda mwingi kujifua ili abaki kwenye ubora wake anatajwa kujiunga na timu ya Mtibwa Sugar ambayo amewahi kuitumikia.
Dida amesema kuwa kwa sasa bado mazungumzo yanaendelea na taratibu zikikamilika atataja timu atakayokwenda.
“Nina ofa tano mkononi kwa timu ambazo zinahitaji saini yangu, zipo nyingine zinatoka Afrika Kusini pia nyingine ni za hapa Bongo, wakati ukifika nitataja timu nitakayokwenda kuitumikia,” amesema.