Kampuni ya simu maarufu nchini TECNO mobile imeongeza mkataba wake na klabu bingwa ya England yenye makazi yake jijini Manchester, yaani Manchester City.
Mkataba huo umesainiwa nchini India huku mafanikio yakionekana katika ushindi wa mabao 4-1 kwenda fainali dhidi ya West Ham kutoka London katika mashindano ya ASIA.
Ushiriakiano na klabu ya Man City unalenga kufikisha lengo la TECNO kuwaletea furaha wateja wake kupitia Teknolojia katika simu na mambo wayapendayo ukiwemo mchezo wa soka ambao ni namba moja kwa mashabiki wengi zaidi duniani.
Manchester City kwa mara ya kwanza wakitumia jezi za TECNO katika jezi zao uwanjani waliibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya West Ham na kuwa mwanzo mzuri katika huo mkataba mpya.
Mkuregenzi Mkuu wa Kampuni mama ya TECNO, TRANSSION HOLDINGS, Stehen Ha amenukuliwa akisema: “TECNO ina furaha kubwa kwa kuwa brand yetu itavaliwa na Manchester City katika mashindano ya Asia na tunaamini ari yetu ya ushindi pamoja na rangi ya blue vitasaidia kushinda.”
Pia kufuatia ushirikiano huo uliosainiwa nchini India katika mjini Delhi, Makamu rais wa ushirikiano katika klabu ya Manchester City, Damian Willoughby alisema: “Manchester City inayo furaha kutangaza rasmi kuwa mkataba uliosainia kwa mara ya kwanza 2016 umesainiwa tena na kampuni inayoongoza Afrika na Asia TECNO. Tumeshirikiana nao kwenye mambo mengi ya mpira na biashara ni jambo zuri kua tunaendelea nao tena hasa katika mashindano haya ya Asia kujiandaa na ligi kuu.”
Baada ya Machester City kutoa kipondo cha mabao 4-1 kwa wagon ha nyundo hao wa London, yaani West Ham saa inatarajia kushuka dimbani katika fainali ya Asia ikiwa na uzi wa TECNO kwa mara nyingine tayari kupepetana na wabishi Wolveshampton nao kutoka England.
Mechi hiyo ya fainali Manchester City wakiwa na uzi wa TECNO inatarajiwa kuchezwa kesho Jumamosi katika jiji la Nanjing nchini China.