Uncategorized

MABINGWA WA KOMBE LA SHIRIKISHO SIMBA WAPOKELEWA DAR LEO

admin August 3, 2020 8:47 am
KIKOSI cha Simba kimewasili leo jijini kikitokea Sumbawanga ambapo kilikuwa na mchezo wa fainali dhidi ya Namungo FC. 

Simba iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 mbele ya Namungo Uwanja wa Nelson Mandela hivyo wamerejea na taji la Kombe la Shirikisho. 

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa wamerejea rasmi mjini kuendeleza shangwe la ubingwa walioutwaa Sumbawanga. 

“Mabingwa kama mabingwa tumerejea kuendelea na furaha kwa kuwa tumeshinda na tumerudi sasa kuendelea na furaha yetu Dar.

“Mashabiki ni ngao yetu kubwa wamekuwa nasi bega kwa bega hivyo mambo mazuri yanakuja na tunafuraha kufikia malengo yetu,” amesema. 

Wachezaji wa Simba wamepanda kwenye basi rasmi lililoandaliwa wakiwa na mataji mawili la Ligi Kuu Bara pamoja na Shirikisho wakiwa Kwenye msafara kuelekea Msimbazi.

TSHABALALA ANA MKWARA ETI AKAFANYIWE VIPIMO VYA MABEGA KISA KUNYANYUA MATAJI, LEO WANATIA TIMU DAR WAKATI WA USAJILI, MIKATABA IWE MWONGOZO WA MAISHA YA BAADAYE

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply