Home Uncategorized NYOTA SABA MATATA WAMPASUA KICHWA MBELGIJI WA SIMBA

NYOTA SABA MATATA WAMPASUA KICHWA MBELGIJI WA SIMBA


KOCHA Mkuu wa Simba, Patrick Aussems amesema kuwa mchezaji atakayeonyesha juhudi mazoezini ndiye atakayepewa kipaumbee kwenye kikosi cha kwanza.

Simba imeweka kambi nchini Afrika Kusini ambapo inaendelea na mazoezi kwa ajili ya msimu ujao huku vipaumbele vikubwa vikiwa ni kufanya vema michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kutetea taji la Ligi Kuu Bara.

Aussems ambaye anaaminika kutumia sana viungo kutafuta matokeo msimu ujao atapusa kichwa kuwachezesha nyota saba ambao wapo ndani ya kikosi hicho na wote wana uwezo wa kucheza nafasi ya kiungo.

Nyota hao ni pamoja na Hassan Dilunga, Clatous Chama, Sharaf Eldin, Francis Kahata, Ibrahim Ajib, Mzamir Yassin, Said Ndemla.

Kahata ambaye ni nyota mpya akitokea Gor Mahia ya Kenya amesema kuwa suala la kuchagua nani aanze anamuachia kocha kwani yeye ndiye anayepanga kikosi.

SOMA NA HII  BREAKING:KIWIKO CHAMPELEKA MORRISON KAMATI YA NIDHAMU