REKODI ya Gareth Bale akiwa ndani ya Real Madrid inavutia, amecheza jumla ya mechi 231 na kupachika mabao 102 huku akitoa pasi za mabao jumla ya 65.
Kwa upande wa mataji ametwaa Ligi ya Mabingwa makombe manne sawa na Super Cup huku akibeba La Liga, Copa Del Rey, Supercopa De Espana mojamoja kwa sasa anatakiwa aondoke na bosi wake Zinadine Zidane.
Meneja wake huyo amemwambia Bale kuwa lazima aondoke ndani ya kikosi hicho ili aache furaha kikosi hapo.







